Tundu Lissu Afanyiwa Upasuaji Kubwa Mara 17, Atolewa ICU

Tundu Lissu Afanyiwa Upasuaji Kubwa Mara 17, Atolewa ICU
 Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe amesema kuwa Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu ametoka ICU na sasa anaweza kukaa.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Jumanne, Mbowe amesema afya ya Lissu inaimarika kwa kuwa alihitaji upasuaji mwingi sana kutokana na risasi zilizoingia kwenye mwili wake.

“Amefanyiwa upasuaji mkubwa mara 17 mpaka sasa. Ameongezewa damu nyingi kuliko mtu yeyote miaka 20 iliyopita ametoka ICU wiki iliyopita,” amesema Mbowe.

Soma: Mbowe: Lissu anaweza kuongea na kula kidogo

Amesema Lissu hatumii oxygen tena wala mirija na kwamba anakula chakula anachokitaka.

“Juzi kwa mara ya kwanza alikaa, anatembea Wheel Chair na aliliona jua kwa mara ya kwanza,” amesema Mbowe.

“Tunawashukuru madaktari wa Dodoma na Nairobi. Hospitali ya Nairobi imefikisha awamu ya pili ya kutibu. Tunavyozungumza baada ya wiki moja kadri madaktari watakavyoshauri atamaliza matibabu ya pili,”

“Ataanza awamu ya tatu nje ya Nairobi yatakayokuwa ya muda mrefu. Kwa usalama wake hatutataja wapi anakwenda. Siyo Tanzania na sio jirani. Hiyo ndio hali halisi ya mgonjwa.”
Tags

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Eti kwa usalama.......wakuogopewa ni wewe, unafahamu kila kitu

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad