VIDEO: Mwili wangu ndio biashara yangu – Calisah


Mwanamitindo anayekuja kwa kasi nchini Tanzania, Calisah amesema kwa sasa anajifua na mazoezi ili kuutengeneza mwili wake uwe wa kibiashara zaidi kwa ili uvutie watu wanaotaka kufanya nae kazi za matangazo.

Hata hivyo, Calisah amesema kuwa kitendo cha yeye kupata matangazo mengi na kuonekana kwenye mabango kinamfanya ajiweke vizuri kwa kufanya mazoezi ili awe na muonekano wa kijasiri huku akikataa kuwa hafanyi mazoezi kwa ajili ya kupendwa na mademu.

“Mimi biashara yangu ni mwili wangu kama ambavyo ukiuza nguo mtaji wako ni nguo, Mgari magari ukiuza gari lazima u-invest kwenye magari mengine, mimi kazi yangu ni Modo watu wamezoea kuniona kwenye Tv kwenye mabango kwenye runway hivyo lazima nijiweke fiti“,amesema Calisah



Kwa upande mwingine Mwanamitindo huyo amesema kuwa mwaka huu ameamua kuachana na fani hiyo ya mitindo na kuingia kwenye masumbwi.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad