Wadukuzi wa Korea Kaskazini Waliiba siri za Kijeshi za Korea Kusini

Wadukuzi wa Korea Kaskazini Waliiba siri za kijeshi za Korea Kusini
Wadukuzi kutoka Korea Kaskazini walidukua mitambo ya kijeshi ya Korea Kusini na kuiba nyaraka nyingi zenye taarifa muhimu za kijeshi.
Miongoni mwa yaliyokuwemo kwenye nyaraka hizo ni mpango wa kumuua kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong-un.

Mbunge wa Korea Kusini Rhee Cheol-hee amesema taarifa hizo zilitoka kwa wizara ya ulinzi ya Marekani.
Nyaraka hizo zilikuwa na mipango ya karibuni zaidi ya kijeshi kati ya Korea Kusini na Marekani.
Kwa Picha: Maisha taifa lenye usiri zaidi dunaini

Mwanafunzi anayetaka ukasomee Korea KaskaziniKorea Kusini mwezi mei ilifichua kwamba sehemu kubwa ya data iliibiwa na wadukuzi Septemba mwaka jana, madai ambayo Korea Kaskazini ilikanusha.
Jeshi la Korea Kusini limesema kufikia sasa asilimia 80 ya taarifa ambazo ziliibiwa kufuatia udukuzi huo bado hazijatambuliwa.
Mambo muhimu kuhusu hali ya kijeshi rasi ya Korea

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad