Mahakama ya juu nchini Kenya itatoa uamuzi wa muda wa mwisho kuamua iwapo marejeleo ya uchaguzi wa urais yanaweza kufanyika siku ya Alhamisi.
Mahakama hiyo itasikiza ombi la dharura siku ya Jumatano kuhakikisha kuwa uchaguzi huo unafutiliwa mbali siku moja kablka ya kufanyika kwa uchaguzi huo.
Hatua hiyo inajiri baada bya mahakama hiyo kufanya uamuzi wa kihistoria ilipofutilia mbali matokeo ya uchaguzi wa urais na kutaka uchaguzi huo kurejelewa.
Sasa inatakiwa kuingilia kati kwa mara nynegine na itaamua , ikiwa imesalia chini ya saa 24 kabla ya uchgauzi huo kufanyika kuhusu iwapo uchaguzoi huo unafaa kuendelea.
Kuna utata kati ya sheria za uchaguzi, katiba na vile mahakama ilivyofafanua sheria hizo.
Kiongozi mkuu wa upinzani Raila Odinga ametumia mojawapo ya uamuzi wa mahakama kujiondoa katika uchaguzi huo akiutaja kuwa usio huru na haki na hautatoa maono ya Wakenya.
Rais aliyepo sasa Uhuru Kenyatta amesema kuwa uchaguzi huo ni sharti ufanyike, huku akiwa na muswada wa uchaguzi katika meza yake unaotarajiwa kutiwa saini
Mahakama ya juu imekubali kusikiliza ombi hilo la muda wa lala salama ambalo linahoji iwapo tume ya uchaguzi na mwenyekiti wake wataweza kufanya uchaguzi ulio huru na haki siku ya Alhamisi.
Inataka uchaguzi huo kubadilishwa na uchaguzi mpya hatua ambayo huenda ikaongeza muda wa uchaguzi huo kwa kipindi cha mwezi mmoja .
Wapiga kura watatu wameelekea katika mahakama ya juu wakitaka kusimamisha uchaguzi huo wa Alhamisi.
Bwana Khalef Khalifa , Samuel Mohochi na Gacheke Gachuhi wanadai kwamba tume ya uchaguzi imegawanyika na haiwezi kufanya uchaguzi ulio huru na haki.
Wanadai kwamba makamishna wa IEBC wanahudumu kwa upendeleo na mwenyekiti wa tume hiyo Wafula Chebukati amekiri hadharani kwamba hawezi kusimamia uchaguzi ulio huru na wa haki.
Walalamishi hao watatu ,wanaowakilishwa na Harun Ndubi pia wanataka mahakama kuamua kuhusu hatua ya Raila Odinga kujiondoa katika uchaguzi huo.
Wanavyoelewa ni kwamba hatua ya Raila Odinga kujiondoa katika uchaguzi huo inamaanisha kwamba uchaguzi huo unafutiliwa mbali.
Wanahoji kwamba ilani ya gazeti rasm la serikali lililotangaza uchaguzi huo imepitwa na wakati kufuatia hatua hiyo ya Odinga.
Wanadai kwamba tume ya IEBC huenda isiweze kusimamia uchaguzi huo kama ilivyoagizwa na mahakama ya juu kutokana na maadalizi hafifu.
Kuna hatari kwamba uchaguzi huo huenda usifanyike katika idadi kubwa ya kaunti hatua itakayoweka hatma na maisha ya Wakenya katika matatizo.
Watatu hao wameagizwa kuwakabidhi wahusika agizo la kesi hiyo kufikia saa kumi na mbili jioni.
Rais Uhuru Kenyatta alisema kuwa ijapokuwa hakubaliani na uamuzi wa mahakama ya juu ana uheshimu
Rais Uhuru Kenyatta alisema kuwa ijapokuwa hakubaliani na uamuzi wa mahakama ya juu ana uheshimu
Wakati wa kuchapishwa kwa taarifa hii wakili wa rais Uhuru Kenyatta Tom Macharia na wale wanaowakilisha IEBC walikuwa washakabidhiwa agizi hilo.
Wakitoa uamuzi wao manmo tarehe mosi Septemba, majaji sita wa mahakama ya juu waliunga mkono ombi lililowasilishwa na Raila Odinga kwa majaji 4-2 aliyedai kwamba mfumo wa kielektroniki ulidukuliwa na kuingiliwa kwa lengo la kumsaidia rais Uhuru Kenyatta.
Uhuru Kenyatta alitangazwa mshindi wa kura hiyo kwa asilimia 54.
Majaji hao walisema: Tume ya uchaguzi ilishindwa ama hata kukataa kufanya uchaguzi wa urais katika hali ambayo inalingana na katiba .
Hatahivyo mahakama hiyo haikumlaumu rais Kenyatta ama hata chama chake.
Kenyatta alisema kuwa anajutia kwamba watu sita wameamua wataenda dhidi ya matakwa ya raia lakini hatopinga uamuzi huo.