Wakili Anayemtetea Lema Katika Kesi ya Kumtukana Rais Magufuli Ajitoa Ghafla

Wakili Anayemtetea Lema Katika Kesi ya Kumtukana Rais Magufuli Ajitoa Ghafla
WAKILI Sheck Mfinanga, anayemtetea Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema, katika kesi ya kumtukana Rais John Magufuli, amejitoa ghafla.

MBUNGE WA ARUSHA MJINI, GODBLESS LEMA.
Kujitoa kwa wakili huyo kulimfanya Lema aiombe mahakama kuahirisha kesi hiyo hadi siku nyingine, ili apate muda wa kumtafuta wakili mwingine.

“Mheshimiwa Hakimu, mimi ni mbunge na ni mwanasiasa; si wakili, hivyo kujitoa kwa wakili wangu kumenishtua, naomba muda zaidi nitulize akili kisha nitafute wakili mwingine na nikimkosa nitajitetea mwenyewe,” aliomba Lema.

Baada ya ombi hilo, Hakimu Desderi Kamugisha aliwahoji mawakili wa serikali ambao ni Khalili Nuda na Alice Mtenga ambapo,
Nuda aliieleza mahakama kesi hiyo ilipangwa kuanza kusikilizwa ushahidi wake jana na Wakili Mfinanga amejitoa, hivyo ni haki ya mshtakiwa kupewa muda Zaidi, ili atafute wakili mwingine.

Wakili Kamugisha alikubaliana na ombi la mawakili wa serikali na Lema na kuongeza muda hadi Novemba 14, mwaka huu.
Kesi hiyo ipo Mahakama ya Wilaya ya Arumeru.

Wakili Mfinanga alidai hataweza kuendelea kumtetea mteja wake kutokana na kushindwa kupata mwenendo wa shauri hilo licha ya kuomba mara tatu, ili aweze kukata rufani Mahakama Kuu.

Kujitoa kwa Wakili Mfinanga kulifanyika mahakamani hapo kabla ya kuanza usikilizwaji wa kesi inayomkabili mteja wake ya kutoa matamshi mbalimbali ya kumtukana Rais.

Alisema: “Ninaomba nijitoe kuendelea na kesi hii sababu nimeomba nakala ya mwenendo wa kesi zaidi ya mara tatu.

“Leo hii (jana) pia nimeomba, ili nimsaidie mteja wangu kukata rufani, hakimu umeninyima sasa kwa misingi hii naomba kujitoa na sipo tayari kuendelea kumtetea.”

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad