Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amefunguka na kusema kuwa wapo watu ambao walikuwa ni wezi katika Chama Cha Mapinduzi (CCM) na kusema saizi watu hao wamekimbilia Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA).
Rais Magufuli amesema hayo leo Oktoba 31, 2017 akiwa ziarani mkoani Mwanza ambapo alikuwa akiongea na wananchi wa Mkuyuni na Butimba jijini Mwanza na kusema kuwa yeye anataka maendeleo kwa kuwa anaamini Tanzania inahitaji kujengwa na Watanzania wote na kudai ndani ya vyama vya siasa kuna wezi ambao hao ndiyo wamechelewesha maendeleo ya nchini.
"Tunataka Tanzania mpya hilo ndiyo lengo langu kwa sababu yapo yalikuwa ni majizi makubwa sana Chama Cha Mapinduzi (CCM) yakakimbilia CHADEMA ndiyo maana sijasema CUF oyeee kwa sababu wapo waliomo CUF wengine ni wabaya sana. Mimi nataka maendeleo kwa sababu maendeleo yanaletwa na Watanzania wote tushikamane ndugu zangu tutachelewa tushikamane sasa hivi tuipeleke Tanzania yetu mbele" alisisitiza Rais Magufuli
Wale Majizi Makubwa Waliokuwa CCM Wanakimbilia CHADEMA- Magufuli
13
October 31, 2017
Tags
Majizi makuu ni ya ESCRzoW, IPTL, waliosaini mikataba mikuu mibovu ya madini wapo huru raisi wangu. Wengine ni miongoni mwa maraisi waliopita kabla hawajawa maraisi. Leo unasema na unauliza viwanda vipo? Unamjua nani kiongozi mkuu wa nchi hii aliuza viwanda na mabenki. Na majumba ya serikali walijiuzia. Mbona huwatumbui hawa. Ni wao waliokuwa huru wakiwa wakijitafutia madlahi binafsi, watoto wao, marafiki na kila aliyekuwa madarakani. Hawa hujawagusa bado. Je tutegemee nini huku kutumbua kwako bila katiba itakayolinda maslahi haya. Je kna tofauti gani kati yako na viongozi wastaafu bila katiba. Na mliokuwa madarakani mbwembewe zote hazitalindwa, wala hakuna mtu ambaye atapelekwa mahakamani kwa uongozi wa juu sababu bado mna kinga. Badala ya kutenda huku na kule kuwafurahisha watu, watanzania wanahitaji katiba na usilidharau hili. Wape watanzania katiba kwanza badala ya kuwasema mafumbo viongozi wa msimu uliopitaamba maraisi waliruhusu chini ya uongozi wao.anza na hao ambao ni chanzo cha matatizo yote haya. Tumbua mapapa kwanza halafu uje kwa vidagaa.
ReplyDeleteHahaaaaaa mbona wakitoka ndio wanaitwa wezi .tumeshaelewa.
ReplyDeleteMijizi ya mali asili na utalii, ipeleke tu mahakamani hata kama imekwenda kujificha kwenye vyama vya siasa.
ReplyDeletembona Mkapa hamtaji? bado anajifanya rafiki yake, kumbe imemuuma.
ReplyDeleteMaraisi wote waliopita ndo waliitupeleka huko. Unachokitumbua ni matokeo ya maraisi toka ccm ambao waliachia uhuru, walijipa mali wenyewe, na wafuasi wao kushirikiana. Wapinzani wamesema moja kwa moja tymbua hao bila kuogopa. Leo unabeza watu wanaohsma . Wapinzani na watanzania wanataka katiba kusudi usiwalinde hao. Na unakula nao bado sahani moja. Kama tumbua ni halisi na kweli, weka vigogo wakuu waliohusika na haya yote amba ni maraisi. Kama mawaziri walipewa ok na mkubwa kama ok inavyofanywa sasa toka juu. Utamtumbuaje aluyepewa amri ukamwacha mwenyewe. Tusitaniane danganyane, na kufanyia mchezo Taifa hili. Kama ni ushujaa basi jitose nahao mapspa, weka katiba, hakuna wa kupona . Taifa lianze upya na nguvu mpya bila upendeleo. Si hii fukia fukua kama bata. Uliahidi hutamwogopa mtu. Haki, usawa na sheria moja itawale nchi. Bado sijsona hili. Unawafurahisha wachache tu wasiozamia na kutaka Tanzania mpya. Na si hao akina mama wanaokuja kukulilia ukiwa jukwaani. Wanakuja sababu sheria na viongozi bado wsnyanyasaji, bado wanapokea rushwa. Na wengi wso ni ccm wsliona vyeo, wakuu wa mikoa, wilaya na wanasheria wa ccm.ni dufu bado linatafuna nchi na kudhurumu watu. Ni ccm iliyo madarsksni bado inatoa vyeo kwa walarushwa. Kama mnania hawa wenye tuguma bado wako ccm mbona unawapa vyeo. Hii inachanganya wananchi bado. Mla rushwa wa ccm annebarikiwa na kupanda cheo akitoka mwizi. Haya macho yanaona upinzani tu. Msililigawe taifa zaidi ys hapa ni hatari sana.
ReplyDeleteMuuaji huyo
ReplyDeleteNi mmjawapo wa majizi. Msitete ujinga, hapa ni kuangalia mustakhabali wa Taifa Sio siasa uchwala la bara hili lonalimaliza hili bara, bara haliendelei hataaa, kwa ajili ya korruption kila konaa, mwacheni raisi awabane ndio maana wanatapatapa hawaoni pa kushika, walishazoea wizi,ufisadi wa kila aina, hiii Dar es salaam yenyewe haileweki, huko vijijini ndio hoi bin taabani kwa ajili ya viongozi wabovu, Sasa raisi wa Sasa kaguswa mwacheni afanye kazi yake aliyopewa, madam akuja kuiba wala kufanya ufisadi na kuendelea kuiangusha nchi, wake up people, hebu wengine jaribuni kuzunguka zunguka mkiwa na vijihela vyenu, Lakini Sio vya wizi au ufisadi na muone nchi za wenzenu muone zilivyo mtaona aibu kabisaa, sura ya nchi Sio vijumba vywenu vizuri tu, na mazingira, barabara nzuri, miundo mbinu ya kueleweka, huduma za afya, Elimu, alafu hawana marumbano marumbano ikiwa kitu ni kwa manufaa ya Taifa, Sasa huku mijitu imekalia uchoyo, wivu, majungu,wivu, kuiba kufisadi ndio hivyo inatapika tu hovyo, stupid Africa mentality
ReplyDeleteNakubali majinnga Africans ndiyo. Majinga Africans hayawezi kumkosoa raisi mwizi, fisadi,. Hayawezi kuuona ukweli. Mimi sikatai utumbuaji, lakini kwa nini watanzania mnajua hasa ni kuanzia enzi za Mkapa na kufikia Kikwete ilikuwa kazi as usual kuiba. Na kwa nini mnawaogopa wasitumbuliwe. Ni hawa vyanzo vya haya yote ambayo ndugu Magufuli anajaribu kuyafagia. Lakini huwezi kufagia mkia wakati kichwa bado. Hivi mbona mnakuwa ndumila kuwili. Akina Kinana na meli za meno ya tembo. Mkapa mtaifishaji viwanda, beki, madini, na aliyesaini dhahabu ni raisi aliyemfuata, lakini alisaini mikataba kabla. Mmmekaa kimya. Haya yote yanayotumbuliwa leo ni wao ndo nguzo na chanzo. Hivi ubishi na majungu haya yote, pamoja na elimu zote , mnawalinda. Na waarabu waliokuja mbugani kushika wanyama na kutorosha walitumia kibali cha raisi. Haya yote yapo hadharani, sasa mnawatumbua waliotumwa tu. Dingi mnamkalia kimya. Je mnataka mabadiliko au utani tu. Waliotajwa na account nje. Kwa nini kama mnahasira msikae meza moja na wapinzani, mkakubaliana kwa manufaa ya watanzsnia na kulijadili ni nini chanzo cha haya yote. Mtakuta ni viongozi wakuu wa nchi hii. Watu hawakatai kutumbua. Lakini acheni siasa za midomo, na muiache sheria ifanye kazi. Tatizommnamwona raisi kama mwanasheria.watu wanataka katiba kusudi si raisi adimame kwrnye majukwaa aseme wezi wanakimbia wakati amekataa kuirudisha katiba ili sheria zifanye kazi bila mwingiliano. Haya ni makosa mengine mnayomkubalia raisi azidi kuchukua hukumu mkononi na si kazi yake. Wengi tunaamka ili tujue kazi za raisi ni nini, jeshi ni zipi, mahakama ni zipi. Lakini bado mtu mmoja anaingilia kila kona na huu ni ukiukaji wa sheria pia. Lini watanzania wote tutadai ni muda katiba mpya iingizwe ili tuache kuumizana vichwa namna hii. Na kwa bila woga wote, narudia wote bila kujali cheo cha mtu, kama amekiuka awe hajui sheria au anapuuza sheria anapokuwa kiongozi na kuapa ajue asipofuata seria awe raisi au si raisi ajue atachukuliwa hatua kali. Lakini bado , tunangojea nini? Na kwa nini mnamtetea raisi.tusiposahihisha hili, yote ni bure. Tunarudia kulekule. Mchawi ni sisi wenyewe watanzania waoga ndo tunaorudisha maendeleo ya nchi hii. Mnawakomoa na kuwaburuta watu wasio na makosa kwa kukosoa, mnawakingia kifua maraisi ambao ni chanzo cha haya yote.ebu ka ka ya kuandika muwe serious enough.ebu watanzania tuache malumbao na tuwe serious at least mara moja kwa manufaa ya nchi nzima. Its sad. Inasikitisha sana kutokufikiri kwa dhati na kuchukua maamuzi magumu kwa manufaa ya watanzania wote. Aceni ucha, acheni ukabila, acheni siasa zisizo na msingi. Nilimsikia Ndugu Mkapa akisema ubinafsi, kasahau leo. Ingewezekana hata yeye akae kimya kwani ni mhusika mkuu wa jambo hili. Hana sauti. Sauti yake imeshajichafua yenyewe wakati yupo kiongozi.wote tunamaukumu sawa acheni upendeleo.
ReplyDeleteRAZARO TWIGA, TUMBILI, KIMA ULIWAPANDISHA NDEGE TUAMBIE ULIWAPELEKA WAPI
ReplyDeleteNani alikuwa raisi. Kibali cha raisi na uhudiano wao na ughaibuni. Mnamwogopa kumtaja kijembe wenu mnaenda kwa wale makinikia. Majembe , maraisi waliotoa vibali mbona mnawaogopa. Sasa mnatumbua kwa staili yake na kutokuiweka katiba ambayo hata wengi wenu leo mlio madarakani mnahitaji fagio, mnaogopa kuipitisha katiba kwani mfanyayo pia hayazingatii sheria. Bado mnalindana. Hawa eote mnaowakamata mnawaonea mkijus maraisi waliowatumikia ndio vinara wa uvunjifu wa sheria zote nchini.kama kweli mko na nia ya nchi hii pitisheni katiba kwanza halafu tukae meza moja tuongee ukweli. Hamtathubutu kamwe. Basi ipitisheni hiyo kwanza tuone kama mazungumzo yataendelea vipi.
ReplyDeleteila ccm ni kichwa cha mwendawazimu duu
ReplyDeleteukikaa na mwizi ukiishi na mwizi na wewe utakuwa nani vile mwizi tu tumechoka sisi na maneno yao
ReplyDeleteInasikitisha sana pale mtu anapokuwa ccm anaonekana msafi na hana dhambi yoyote, lakini akishatoka tu kwenda upinzani anaanza kuitwa mwizi/jizi! Ina maana tukiwa ccm tunafichiana siri za huo wizi?
ReplyDelete