Kundi la kimataifa linalopigania kupigwa marufuku kwa silaha za nyuklia duniani limezawadiwa Tuzo ya Amani ya Nobel ya mwaka huu.
Imeelezwa kuwa kundi hili limekuwa na mchango mkubwa katika kupinga na kupiga marufuku matumizi ya silaha za nyuklia kutokana na madhara yake chini ya sheria za kimataifa hivyo linastahili tuzo hiyo.
Kamati ya maandalizi ya tuz hizo ambazo pia ni waamuzi wa kuu wa mshindi wa tuzo hiyo, imehimiza mataifa mengine yenye silaha za nyuklia kutafuta namna ya kuachana na silaha hizo polepole.