Waziri Mkuchika ambaye leo Oktoba 10, 2017 ameapishwa na Rais Magufuli kuwa Waziri Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora amesema kuwa katika kipindi chake atahakikisha wafanyakazi wanalipwa mshahara kulingana na kazi zao kweli, na wanatumia muda wa kazi kufanya kazi za serikali.
"Kwanza katika kipindi changu nikiwa Waziri kwa watumishi wa Umma, nataka wananchi wanapofika maofisini wawakute maofisini, mara nyingi wengi wanaripoto ofisini baada ya muda wanaondoka wanasema wanaenda kunywa chai, yaani wananchi wanatoka vijijini wanamsuburi mtumishi aje eti ameenda kunywa chai jambo hili kuanzia leo nitasimamia kuhakikisha watumishi wa umma wanashinda kazini kwao ili kila mtumishi wa Umma alipwe mshahara kwa kufanya kazi muda wote" alisema Mkuchika
Aidha Mkuchika amesema kuwa kwa sasa watumishi wengi wa Umma wanalipwa mshahara kamili kwa kufanya kazi robo za serikali jambo ambalo yeye atakwenda kulisimamia na kuhakikisha kuwa watumishi hao wanafanya kazi kamili ili walipwe kulingana na kazi zao kamili.
Mbali na hilo Mkuchika amedai kuwa atakwenda kuongea na Waziri wa Elimu ili ikiwezekana somo la Rushwa lianze kufundishwa kuanzia shule ya awali nchini mpaka vyuo vikuu na kusema watu wamekuwa wakichukua na kutoa rushwa kwa kuwa hawana elimu ya kutosha juu ya athari ya rushwa.
Hongera Mkuchika, Fikra Uliyo Ashiria kuzungumza na Mama Ndalichako Ni FIKRA NZURI NA TUNAIUNGA MKONO ikiwa na Maana na Nia ya KUTOKOMEZA kabisa Rushwa From the ROOT Cause....!!!
ReplyDeleteTunawapongeza Waapishwa. Wizara zimepanguliwa na kuongezwa kutokana na uchambuzi uliofanyika na kuonekana iko Haja ya Sisi kuyafanya haya. Na tumeshayafanya .
Tunacho tegemea na kuona ni Kwamba Ufanisi na Weledi wenu nchicho kilicho tupa msukumo mkubwa.
Nia na Lengo Viko Wazi Ni Kumtumikia Mtanzania na Kuweza Kuboresha Maisha yake na Kumpa Huduma Stahiki kwa Wakati Stahiki na Bila Ulongo Longo.
Kinacho wezekana leo KISILALE Na Bila Usumbufu kinafanyika Ili tuweze kuipeleka Tanzania katika Next Level.
Imani Juu yenu tunayo Uadilifu wenu na Uzalendo wenu Hatuna shaka Nao.
Tunawatakieni Kila la Kheri Katika Majukumu yenu Mapya na kumbukeni Dhamana mliyokabidhiwa ni ya Kumtumikia Mtanzania Bila Kujali
Rangi Yake!
Dini yake!
Ukabila Wake!
Chama Chake!
Tanzania ndiyo Kwanza na UBUNIFU uwe ni Wndelevu.
Ajira na Makazi iwe ni Kipa Umbele.
HAPA KAZI TU..... Hongera Baba JPJM na Mh Kassim Majaliwa.