Waziri wa Afya Atoa Agizo kwa Hospitali na Vituo vya Afya

Waziri wa Afya Atoa Agizo kwa Hospitali na Vituo vya Afya
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mh. Ummy Mwalimu ameagiza Hospitali, na Vituo vya Afya vyote vya Serikali nchini kuanzia October 26 kutoa huduma ya uchunguzi wa Saratani kila siku wakati wa kliniki ya mama na mtoto.

Waziri Ummy ametoa agizo hilo wakati akifungua matembezi ya hisani ya kuhamasisha uchunguzi wa Saratani ya matiti, yaliyofunguliwa katika viwanja vya hospitali ya Ocean Road mapema leo jijini Dar es salaam.
Sambamba na agizo hilo Waziri Ummy amezitaka Hospitali hizo kutenga siku moja kila mwezi kwaajili ya kuchunguza na kufanya matibabu ya ugonjwa wa Saratani ya mlango wa kizazi na Saratani ya matiti.

Aidha Mh. Ummy ameipongeza kazi nzuri inayofanywa na Uongozi wa Hospitali ya Ocean Road katika kutimiza majukumu yake ikiwemo kuongeza vitanda 40 mpaka vitanda 100 kwa gharama zao kwaajili ya wagonjwa wa saratani pindi wanapopata huduma za matibabu ya Chemotherapy.
Kwa upande mwingine Mh. Ummy ametoa rai kwa wananchi wote hususani wanawake kujitokeza kupima ugonjwa huo kwani unatibika endapo utagunduliwa mapema.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad