Wizara ya Ardhi Yafafanua Kuhusu Uwekaji wa Alama za X na Kuvunja Majengo

 Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo Yafafanua Kuhusu Uwekaji wa Alama za X na Kuvunja Majengo
Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi imetoa ufafanuzi kuhusu uwekaji wa alama za X na kuvunja majengo yanayojengwa katika miji bila kibali na katika viwanja vya watu wengine walio na hati miliki za ardhi kwa dhuluma.

Taarifa ya wizara iliyotolewa leo Jumatatu Oktoba 23,2017 imesema kwa wale waliojenga kwenye viwanja vyenye hati za watu wengine kwa nguvu na kuwadhulumu wenye hati miliki haki yao ya kisheria, hatua zitachukuliwa ili kuwarudishia haki wanaostahili.

“Hatutabomoa nyumba ya mtu bali tutaendelea na urasimishaji wa makazi kwa maeneo yaliyojengwa holela ili yawe makazi rasmi na wananchi wapelekewe huduma muhimu kama vile barabara, umeme na maji,” imesema taarifa hiyo.

Wizara imesema, “Muhimu wapewe hati miliki ili ziwasaidie kiuchumi na waweze kulipa kodi ya ardhi... lakini tutazuia ujenzi mpya holela katika miji yetu kwa mujibu wa sheria.”

Taarifa imesema viongozi wote wa wilaya na mitaa wahamasishe wananchi kushiriki kikamilifu katika urasimishaji wa makazi yao kwa faida yao na Taifa kwa jumla.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad