Zitambue Kazi za Nywele Katika Sehemu za Siri


Hivi umewahi kujiuliza kazi ya baadhi ya vitu vilivyopo katika mwili wako?

Kuna baadhi ya vitu viko katika mwili vinaweza kuonekana kama havina kazi (useless) lakini kumbe havikuwapo hapo kwa bahati mbaya.

Nywele za maeneo ya siri imekuwa na baadhi vitu ambavyo umuhimu wake haujatiliwa maanani na watu wengi. Imefikia hatua mpaka wengine wanaziona kama ni uchafu mwilini.

Watu wengi hutumia gharama kubwa na vifaa vya gharama kuhakikisha kuwa wananyoa nywele hizo. Watu hutumia viwembe, wengine hutumia mpaka nta ili kuhakikisha kuwa eneo linalonyolewa nywele hizo linakuwa kama walivyokuwa wakiwa watoto.

Baadhi ya wataalamu wa maswala ya kijamii wanasema kuwa watu hutumia jitihada kubwa kupambana na nywele hizi ikiwa ni sehemu ya utamaduni wao, hasa kwa wale wanaodhani kuwa wameendelea na wanaovaa nguo za ndani zinazojulikana kama ‘bikini’.

Wataalamu wa upasuaji wamegundua kuwa kuondoa nywele kwenye eneo la mwili kabla ya kufanya upasuaji, kunaongeza hatari ya athari na maambukizi katika ngozi.

Imeelezwa kuwa unaponyoa nywele zote ktika maeneo ya sehemu za siri, unaongeza hatari ya maambukizi na huchoche bakteria kuingia ndani ya mwili kupitia vitundu vidogo vinayoachwa baada ya nywele hizo kuwa zimenyolewa.

Vile vile, kunyoa nywele zote za maeneo ya siri huongeza hatari ya maambukizi ya magonjwa ya ngono kutokana na majimaji yanayokuwepo wakati wa ufanyaji wa mapenzi kupenya katika vitundu vidogo vilivyobakia baada ya nwele hizo kunyolewa.

Kunyoa nywele za sehemu za siri kunaweza kukusababishia muwasho na kukuletea kero hata unapokuwa mbele za watu. Hebu fikiria umenyoa nywele za sehemu za siri halafu uko mbele ya mkutano kazini, mara ghafla unapatwa muwasho katika maeneo ya siri na makwapa. Unadhani unapatwa na hali gani? mfadhaiko unaoupata unaweza kukuletea fedheha kubwa.

Nywele za sehemu za siri huwa na kazi ya kuizuia ngozi dhidi ya michubuko, pamoja na bakteria mbalimbali ambao wanaweza kushambulia maeneo nyeti. Vile vile nywele kama za makwapa hudanya kazi ya kufyonza jasho linalotoka ili lisitiririke katika maeneo mengie ya mwili wako.

Uamuzi ni wako. Ikiwa utaamua kunyoa nywele za sehemu za siri ama la, hiyo ni juu yako. Lakini kumbuka kujiweka safi musa wote na kuhakikisha kuwa mwili wako unakuwa nadhivu na wenye afya.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad