Zitto Afunguka Makubwa Baadam ya Rais Magufuli Baada Ya Kukamilisha Majadiliano Kati Ya Tanzania Na Barrick


Ameandika Zitto Kupitia Ukurasa wake wa Facebook:

Mwezi Machi 2017 niliwaambia Watanzania kuwa tumepoteza TZS 1.8 trilioni za kodi ya capital gains kwa maamuzi ya papara ya Rais kuhusu mchanga. Nilitukanwa Sana.
Leo tumeishia kupata TZS 640 bilioni ( 1/3 ya tulichokosa ). Mnashangilia Sana.
Nikiwaita Mazwazwa mnasema nawatukana.
Niliandika Machi 2017

" Amri ya Rais kuhusu 'Mchanga wa Dhahabu' imepotezea nchi Tshs 1.8trn Capital Gains Tax
Jana nilipokuwa natoa mada kuhusu miaka 50 ya Azimio la Arusha niliongelea pia suala la umakini wa viongozi katika kauli zao. Kwamba Kiongozi lazima ujue unatoa kauli gani wakati gani. Niliwaeleza wanachama na wageni wengjne katika mkutano wa ACT Wazalendo kuwa Amri ya kiholela aliyoitoa Rais John Magufuli kuzuia usafirishaji wa Mchanga wa Dhahabu imepelekea nchi yetu kupoteza USD 880m Kama kodi ya ongezeko la Mtaji kutokana na mauzo ya Acacia Mining.

Hivi sasa nchini kwetu kuna sheria ya kutoza 20% ya thamani ya mauzo iwapo kampuni zinauziana hisa. Tozo inayotozwa inaitwa Capital Gains Tax. Kodi hii mpya ilitungwa mwaka 2012 ili kukabili wawekezaji waliokuwa wanauziana makampuni juu Kwa juu bila Tanzania kupata lolote. Tanzania imeshafaidika na kodi hiyo Kwa mauzo mbali mbali ambayo yamekwisha fanyika kwenye sekta mbalimbali.

Wakati Rais anatoa AMRI kuhusu Mchanga wa madini kusafirishwa kwenye nje ya nchi kulikuwa na mazungumzo yanaendelea kati ya Kampuni ya Acacia mining ( yenye Assets zinazozalisha nchini Tanzania tu kwa sasa - Buzwagi, Bulyanhulu na North Mara) na kampuni nyengine ya nchini Canada kuhusu Acacia kununuliwa Kwa USD 4.4bn. Mara baada ya amri hiyo mazungumzo yalivunjika na hivyo mauzo kutofanyika.

Iwapo Rais angechelewa kutoa kauli yake Kwa wiki moja tu mazungumzo yale yangepelekea mkataba wa mauzo kusainiwa na hivyo Serikali ingepata 20% ya thamani ya Mauzo Kama kodi ya Ongezeko la Mtaji ( capital gains tax ). Hivyo kauli ya Rais imesababisha hasara Kwa nchi yenye thamani ya USD 880m sawa sawa na shilingi 1.8 trilioni".
Watanzania amkeni huu usingizi wa pono.

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. hahaha! wapigaji utawajua tu, umetueleza hasara tulopata baada ya JPM kuzuia kusafirisha nje mchanga, hebu tueleze na faida tulokuwa tunapata wakati mchanga unasafirishwa nje........mfyuu...uliahidiwa mshiko kama mchanga ungesafirishwa ama nene?! Ndo'maana wanakukimbia, utabaki wewe na mkeo kwenye act.......tunajua wapinzani kazi yenu kubwa ni kupinga kila kitu afanyacho JPM hata kiwe cha manufaa kiasi gani, NYINYI ENDELEENI KUPINGA TU, SISI na JPM, JPM na SISI tunamuelewa kuliko kawaida............MTANYOOKA TU.....hahaha

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad