Zitto Kabwe Afunguka Mazito Baada ya Kuona Picha na Kusikia Sauti ya Tundu Lissu

Zitto Kabwe Afunguka Mazito Baada ya Kuona Picha na Kusikia Sauti ya Tundu Lissu
Mbunge wa Kigoma Mjini na Kiongozi wa Chama Cha ACT Wazalendo, Mhe. Zitto Kabwe amefunguka mambo ambayo yanaendelea nchini hivi sasa na kusema serikali ya CCM inahangaika kuhamisha mjadala wa watu ambao wameshambulia Tundu Lissu.

Zitto Kabwe amesema kuwa jana alipoona picha za Tundu Lissu na kusikia sauti yake alifarijika kwani sasa anaamini kuwa kiongozi huyo siku za karibuni ataungana na wao katika kuendelea kupambana kujenga Demokrasia ya nchi.
Aidha Mbunge huyo amedai kuwa kitendo cha madiwani kununuliwa na viongozi wengine wa upinzani ni ajenda ya serikali ya CCM kuhakikisha wanazima mazungumzo juu ya watu ambao walifanya shambulio kwa lengo la kutaka kumuuwa Mbunge wa Singida Mashariki Tundu Lissu.
"Yote hayo yanayoendelea, CCM inafanya juhudi kubwa kuhamisha mjadala kuhusu waliokushambulia kwa kununua madiwani na wanachama wa vyama vya upinzani kila siku, wakiubana zaidi Uhuru wa habari, na wakiuzima uhuru wa vyama vya siasa, hawataki kabisa mawazo mbadala ya kututoa katika hali tuliyonayo. Utakaporudi naamini utakuta mengine mengi mapya. Ninafuraha kuwa unaendelea vizuri sana tofauti na nilipokuja kukuona. Tutazidi kumwomba Mola afya yako iimarike zaidi. Tuna kazi kubwa sana mbele ya safari, na kwa hakika ni lazima tuifanye kwani tusipoifanya Nchi yetu itaanguka Kiuchumi na Kidemokrasia, na watu wetu kuendelea kuwa masikini zaidi kuliko ilivyo sasa" alisema Zitto Kabwe

Mbali na hilo Zitto Kabwe aliendelea kusema "Kupigwa risasi wewe ilikuwa ni lengo la waliokushambulia kutunyamazisha. Tumewaambia kuwa hatutanyamaza kamwe. Kama ulivyoniambia ukiwa kitandani kuwa "tumeshashinda. Tutashinda". Hakika ushindi ni dhahiri na ndio maana wanatapatapa kuzuia Uhuru wa mawazo na fikra. Lakini Shambulio la kutaka kukuua limetuonyesha watu wanaoumizwa na 'INJUSTICE' na wasioumizwa nayo. Wengi wasioumizwa na 'Injustice' wanadiriki hata kuhoji kwanini eti tunapaza sauti kuhusu suala lako" alisema Zitto Kabwe
Zitto Kabwe ni kati ya Wabunge ambao waliweza kufika jijini Nairobi kwenda kumjulia hali Mbunge wa Singida Mashariki Tundu Lissu wiki kadhaa zilizopita.

Post a Comment

3 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Nyie wapinzani mnaokerwa na maendeleo endeleeni kuchonga tu lakini wakati CCM itakapokuja kuzoa ushindi wa kishindo 20/20 msijemkasema mmeibiwa kura kwa sabau kinachoendelea hivi sasa ni CCM kutekeleza kwa kile walichokiahidi kwa watanzania wakati wa kampeni na kwa upande wa upinzani kinachoendelea baada ya kushindwa kukabiliana kisera na CCM wameamua kutengeneza mizengwe ya kisingizio cha kuminywa kidemokrasia. Watanzania sio wapumbavu kwani miaka nenda miakarudi walishudia nchi yao ikigigeuzwa shamba la bibi kila aliekuwa na nafasi ya kukwapua alifanya hivyo na kuwaacha watanzania wakitekeseka na hali duni ya maisha katika nchi iliyojaa itajiri wa rasilimmali.Hakuna kitu kinachoitwa demokrasia kinachopigiwa kelele na wapinzani Tanzania. Unataka kuniambia Mbowe ni kiongozi wa kidemokrasia. Mbowe ni baba wa wajinga wa nchi hii na Kwa uhakika kabisa na ukweli halisi kinachoendelea hivi sasa katika siasa za Tanzania kwa upande wa upinzani ni kuendeleza juhudi kubwa za hujuma ndani na nje ya Tanzania kwa Maghuful na serikali yake ili ashindwe kutekeleza azma yake kuiletea nchi hii maendeleo. Zito Kabwe na wapinzani wenzake Tanzania baada ya kukosa cha maana cha kufanya wamegeuka kuwa wanasiasa wa matukio. Wamekuwa wakisubiri au kutengeneza matukio ili wapate cha kusema. Zito Kabwe anatumia hii taarifa yake alioitoa kuhusu Lisu ili kuficha ule uozo unaoendelea katika chama chake. ACT wazalendo inakufa na hii ni kutokana na upumbavu wake Zito kabwe. Watanzania si wapumbavu. Zito kabwe ameachana na Sera za uzalendo kwa nchi na badala yake anaendeleza sera za usaliti kwa nchi yetu. Huu ni wakati wa vita kwa watanzania vita vya kiuchumi na ndani yake wameshajitokeza watetezi wa mapebari kwa kisingizio cha demokrasia. Wapizani wanapomsubiri Lisu kuja kuendeleza mapambano wanayoyaita ya kidemokrasia wahakikishe mapambano hayo yasiwe kivuli cha kuleta fitna na kuhakikisha serikali iliopo madarakani inashindwa kufanya kazi yake ya kuiletea nchi hii maendeleo la sivyo watanzania wenye uchungu na nchi hii tutapambana kufa kuhakikisha kila hujuma tutakabiliana nazo kikamilifu licha ya kisingizio cha kidemokrasia.

    ReplyDelete
  2. Swadakta... Nchii hii tunauchungu nayo.
    Tena mkae mkijua fika HATUTOACHA WAPIUZI KUICHEZEA.
    NIA YA KUONA MAENDELEO UANALETWA KWA AMANI TUNAYO.
    SABABU PIA TUNAYO.
    NA UWEZO MKUBEA TUNAO (WALA HAINA SHAKA)
    NA VIONGIZI MAGIRI TUNAO.
    MSIJARIBU KEA VISINGIZIO .
    TUKO MACHO NA TUKO IMARA.

    ReplyDelete
  3. Hali haipo shwari tusidanganyane kwenye mitandao na tusiruhusu hisia za kivyama kutuendesha kabisa.... By the way usalama umepungua sana kwa viongozi wa taifa letu ni jambo jema ulinzi kuongezwa hasa kwa kipindi hiki... Yaliyo mpata Lissulinaweza likampata mwingine

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad