Zitto Kabwe Aitupia Lawama Serikali Baada ya Acacia Kusema Hawana hizo Dola Milioni 300 za Kuilipa Tanzania

Baada ya Kampuni ya uchimbaji madini nchini, Accacia kudai kwamba haina pesa za kuilipa serikali ya Tanzania kama ilivyodaiwa juzi  na kampuni ya Barrick Gold Mining,  Mbunge wa Kigoma Mjini Zitto Kabwe amefunguka na kusema kwamba Serikali ilikosea kutangaza ushindi mapema.

Akifanya mahojiano maalalumu jana mchana, Mh. Kabwe alisema kwamba alitegemea kauli kama hiyo kutoka kwenye Kampuni ya Accacia kwani siyo mara ya kwanza kwa Kampuuni ya Barrick kutoa ahadi kama hiyo (ameiita kishika uchumba) kwani hata 2016 walipobanwa na bunge kuhusu suala la misamaha ya kodi waliahidi hivyo.

Mh. Zitto amesema kwamba tangu juzi  alishangaa sana kusikia serikali ikisema kwamba "Tumefanikiwa" kwani haikuwa ikizungumza na kampuni ya Accacia bali mmiliki wa kampuni Barrick na kutokana na sheria ya Makampuni Mmiliki kama mmiliki anasimama mwenyewe na kampuni husimama yenyewe.

"Nilitegemea hili kutokea baada ya serikali kutangaza hayo jana. Ni makosa tuliyoyafanya wenyewe. Serikali kutangaza ushindi kwenye mazungumzo waliyofanya na kampuni hiyo yalikuwa ni makosa kwani ni kawaida kwa kampuni ya Barrick kutoa ahadi kama waliyokuwa wameitoa jana na walishafanya hivyo kwa nchi ya Bolivia, na Chille. Serikali inapaswa sasa irudi kukaa mezani na Accacia wenyewe kwa ajili ya mazungumzo".

Kampuni ya uchimbaji madini, Acacia (Acacia Mining) imefunguka na kusema kuwa haina uwezo wa kulipa dola milioni 300 kwa serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ili kutatua mgogoro wa kodi.
Tags

Post a Comment

6 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Mwacheni zito kabwe alaumu kila kitu juu ya serikali kwani uongozi wa chama chake umemshinda kiasi cha kupelekea kile chama kufa .sasa Zito Kabwe asipo ziba udhaifu wake wa kiuongozi kwa kuilaumu serikali afanye lipi jengine? Mwaache Zito Kabwe ailaumu serikali kwa kufukuzwa chadema, mwaache Zito Kabwe ailaumu serikali kwa wanachama wa Act wazalendo kukihama chama kile kutokana na misimamo ya hovyo ya Zito Kabwe hasa baada ya wanachama wanaoikimbia Act wazalendo kubaini kuwa zito kabwe anawapeleka siko. Zito kabwe ni miongoni mwa wapinzani wanaokerwa na maendeleo ya nchi yetu. Mwacheni Zito kabwe ailaumu serikali kwa kuungua moto nyumba yake kule kigoma? Mwacheni Zito kabwe ailaumu serikali kwa kushindwa kuwatumikia wananchi wake wa kidoma akipita akidhurura na kupoteza muda kama mbunge kupambana na serikali ishindwe kuwaletea watanzania maendeleo hasa wanyonge hali bora ya maisha. Siasa za ushabiki zitatuangamiza watanzania kama kweli tunania yakubadilisha hali zetu za maisha kuwa bora, watu kama hawa akina Zito kabwe sio watu wa kuwashabikia hata kidogo. Zito Kabwe anaonekana kutaka kuvivaa viatu vya kipumbavu vya Tundu Lisu kwa hivyo mwacheni Zito Kabwe aendeleze jitihada za kuwaaminisha watanzania yakuwa serikali iliopo madarakani haifanyi lolote la maana kwa maendeleo ya nchi yetu. Watanzania si wapumbavu wanajua kilicho bora na Magufuli kwa ukweli yupo katika ubora wake hasa kama Magufuli pengine kupita hata matarajio ya watanzania na hata mataifa ya kigeni yanamshangaa alikuwepo wapi wakati Tanzania inateseka kwa kila aina ya ubadhirifu. Hongera sana muheshmiwa raisi na serikali yako kwa uongozi uliotukuka watanzania tunakuunga mkono kwa asilimia 200% .Hongera sana Jembe la kazi Magufuli. Aluta continue...Mapambano yanaendelea mpaka kisagike.

    ReplyDelete
  2. Zitto. Akaia Ni hatumtambui kihalali hapa nchini.
    Na Baliki ndiyo mmiliki.
    Na alichosema John Thorton ndicho kitakacho fanyika.
    Ni suala la muda Tu kuomesha ukakamavu.
    Dogo unahitani kujua Kiaki na Mawazo.
    Mbinu tunazijua na Tunazo ikibidi tutafanya ya kweli.
    Chetu kitatoka na HAKILIKI

    ReplyDelete
  3. Uzito yajua usiyaungumzie.
    Umetumwa??

    ReplyDelete
  4. Heee.! Huyu ndiyo msemaji ya hawa magumashi akasia..??
    Laki payroll take imaidhinishwa Na nani? Anasema ameamza nao kazi kule chile Na wapi kule mwingine.

    ReplyDelete
  5. Wayanzania tunamatatizo gani kielimu. Hivi mnapochangia haya mambo mnayaelewa au la. Je mnajua mikataba ya kimataifa na ujanja wa mabepari. Msiandike kama elimu zenu hazina elimu hii. Zitto ni mmoja wa kumuunga mkono katika sakata hili. Haya makampuni ya nje ni majanja. na kama Watanzania wengi mnadiriki kumsema Zitto ambalo analolisema ni sahii basi wengi Watanzania ni wajinga. Sababu kama si mtaalam wa mambo kaa kimya. Bariki na hili kampuni jingine ni kitu kimoja. Wanajua Afrika bado hawajaamka. Kama hawana pesa then take over. usimbembeleze pepari mwizi na njanja. kazi yake kila siku ni kuangalia wapi wamelala apate. Na Tanzania bado tumelala. Haya makubaliano yote ni mbwembwe na kununua muda. Mkumbuke bado wanachukua dhahabu. haya ni masalia ya dhahabu. Hivi kwa nini wengi hatuna akili za kufikiri.
    tena mnakubali kugawana baada ya kutoa matumizi. mnagawana faida, mnaujua ujanja wa makampuni yote mageni wanavyotumia mikopo inayotolewa na benki kuu ya dunia kujitangazia hasara? Je mnajua mishahara yao mikubwa kiasi gani? Mnajua kila safari wanayokwenda kokokote ni hasara hata ikiwa ya kibinafsi inaingia kitabuni. Wengi msiosomea uchumi msiseme kitu sababu hmjui hivi vitu. Waacheni wenye uzoefu na wafanya biashara wanazijua loopholes nyingi na inakuwa vile sababu ya kuonyesha faida chache au hakuna faida kabisa.
    hii si mambo ya profesor kufuatilia ambaye ni mwalimu tu. Yupo hasa kwenye theory, mleteni mtendaji vitu tuendane kimazungumzo. Mnaingiza mabepari makubwa bila kujiandaa kikamilifu matokeo ndio haya.Mnashangilia mmeshinda wanakuja wanasema sawa, toka mabilioni ya malimbikizo mpaka kwenye mamilioni , na bado wasema ahha hatuna pesa pesa. So what next?Msiingize siasa kwa kumbeza Zitto sababu ya chama. Nyinyi wanaCCM ndio tatizo kuu linaloikwamisha nchi hii.
    Lisu aliwaambia suala la sheria si la siku moja kulipitisha bungeni. Hazijapita siku nyingi lile jambo alilolisema lissu ambaye wengi walidhani mpaka sasa angekuwa marehemu na haya yote yasahaulike. Mungu anawapenda Watanzania Lissu bado mzima, na kauli yake kuhusu sheria ya dharula ipo hapa. Watanzania Amkeni fungukeni macho mjisomeshe na kupjipatia elimu za kuwakomboa wenyewe badala ya kungojea fulani. Kila Mtanzania akitimiza wajibu wake sawa taifa litasonga mbele sana . lakini kama wengi wetu ni wajinga ndo hivi tunashindwa kuzilinda mali zetu.

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad