Zitto Kabwe Awapa Makavu Wanachama wa ACT Wazalendo

Zitto Kabwe Awapa Makavu Wanachama wa ACT Wazalendo
Mbunge wa Kigoma Ujiji ambaye pia ni kiongozi wa chama cha ACT- Wazalendo, Zitto Zuberi Kabwe, amewataka wanachama ambao wanaamini chama hicho ni jukwaa la kuitetea serikali, kutoka ACT Wazalendo kwani sio mahali sahihi kwa wao kuwepo.

Zitto Kabwe ameyasema hayo leo alipokuwa akizungumza na waandishiwa habari katika ofisi za chama zilizopo Kijitonyama jijini Dar es salaam, na kusema kwamba kama watu hao wapo ndani ya chama, ni vyema wakaondoka kama walivyofanya wanachama wengine walioondoka ACT-Wazalendo.
“Tunawaasa wote wanaodhani kuwa chama hichi kitakuwa jukwaa la kuisifia chama tawala na serikali, hili sio jukwaa sahihi kwao, wajitathimini ama kuendelea na uanchama au wajivue kama walivyofanya wenzao”, amesema Zitto Kabwe.
Kauli hiyo ya Zitto Kabwe imekuja siku chache tangu aliyekuwa Katibu Mkuu wa Chama hicho Samson Mwigamba, kujiunga na chama cha CCM

Post a Comment

3 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Angry �� face.
    Zitto Una miguu miwili.
    Una Vichwa viwili.
    Na Nwele salasini na mbili.
    Kilicho nishinda Ni kujua Una akili ngapi?
    Manaake vichwa viwi inawezekana ikawa either Mimi ka Ni full au PIA inawezekana ikwa huku nusu na kile nusu.
    Hebu tueleze vipi mgao WA hapo?
    Je wewe kichwa maji Una wasiwasi na Utendaji WA awamu hii ya Tano??
    Ndiyo Maana wakaondoka.
    Sauri yako funhuo nnazo Mimi .
    Ikiwa WA mwisho kufunga mlango WA ekti. Itanidi uusindike Tu.
    Hovyooooo!!
    Mirembe ulisha kwenda?
    Nakumbuka faili lako lilikuwa huu...USIFANYE MASIHARA NA AFYA YAKO DOGO...
    HAPA NI KAZI TU.
    MLIOPITWA N wakati kuleeee...NJEEE

    ReplyDelete
  2. Zito kabwe awapa makavu wanachama wa Act wazalendo? Katika siasa za Marekani kuna vyama vingi vya siasa ndaniyake lakini vyama viwili vikubwa ndivyo vyenye mguvu kiasi kwamba kuonekana duniani yakuwa Marekani kuna vyama viwili tu vya siasa yaani Democrat and Republican. Democrat ina nembo yake ya utambulisho yaani alama ya Punda hapana shaka ni alama ya kuwajali wanyonge. Na Republican wana nembo yao maarufu yaani alama ya Tembo na hapana shaka ni alama ya kumaanisha nguvu ikiwa ni nguvu ya chama au kuwajali watu wenye nguvu kama vile matajiri au kuendesha shughuli zao za siasa na kiutawala kwa kutumia mabavu .Vyama hivyo vimekuwa vikiishi kwa matendo ya ukaribu sana wa majina na alama zao.
    CCM ni chama kama ilivyo jina lake na nembo yake ni chama cha mabadiliko au mapinduzi ikiwa ya kimaisha au ya kiuongozi na kimfumo pamoja na kuwajali wanyonge. Hata yale mabadiliko ya kisera na mkakati wa chama wa kujivua gamba pamoja na kumpitisha Magufuli baada ya Lowasa kugombania uraisi hayakutokea kwa bahati mbaya ndani ya CCM ni moja kati ya maleno ya uasisi wake. CCM ni chama cha mapambano ikiwa ndani ya Tanzania au Africa kwa hivyo wanasiasa wetu wa ndani kama watakuwa wazuri katika historia ya nchi yetu na Africa wajue kupambana na CCM kisiasa ni kupambanana na mshindani asiekata tamaa mpaka mwisho wa mechi. Kuhusu Zito na chama chake cha ACT wazalendo? Watanzania walikitarajia chama hicho kuwa chama cha kizalendo na kujali uzalendo hasa pengine kuliko hata CCM ya Maghuful. Kilitarajiwa kuwa mbadala wa CCM sio chadema . Chadema hakiwezi kutawala Tanzania kama hakitabadilika kimfumo na kiutawala . Watanzania wemgi wanakiona chama cha chadema ni chama kilichokuja kuwagawa na kwa watanzania kugawa kisiasa au kimajimbo ni kitu ambacho wanakichukia kuliko hata mgawiko wa ndoa zao.Lakini kwa ACT wazalendo wanachokishuhudia hivi sasa watanzania ndani ya chama kile ni "kulinajisi"neno uzalendo. Kwa kuwa matendo na kauli za Zito Kabwe ambae kwa sasa ni kiongozi muandamizi wa Act wazalendo ni dhahiri ni vya kulisaliti taifa mchana kweupe sasa nini maana ya kuitwa chama cha wazalendo? wakati chama kina mikakati ya kulirudisha nyuma taifa? Waache wenye akili zao wakihame kile chama na wasipomtimua zito kile chama kitapotea kusikojulikana kilipokwendea . Nadhani Zito Kabwe ataendelea na madai yake yakwamba watu wasiojulikana wamekipoteza chama chake lol, wakati ni yeye mwenyewe kushindwa kwenda na mabadiliko na kasi ya CCM. Wanasiasa wetu wa upinzani bado wanaiishi wakati wa mkapa na kikwete kitu ambacho kitawagharimu sana kisiasa utakapokuja uchaguzi mkuu.

    ReplyDelete
  3. Swadakta wadau hapo juu.
    Mimi kikwelo Na wasiwasi nae huyu kijana.
    Manakee huwa simwelewagi huko FB Na server anayotumia.
    Naona Kama anaharibikiwa kiakili Na kimaisha.
    Hajui aanze wapi au ashike wapi.
    Anahitaji msaada. Tena hv sasa anafamilia Na kadogo pia.
    WASAMARIA WEMA MPOOOO.
    KASI YA MAGU NA UTENDAJI HAIWEZI.

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad