Ado Shaibu: Jeshi la Piolisi Limechukua Simu ya Zitto Kabwe

Ado Shaibu: Jeshi la Piolisi Limechukua  Simu ya Zitto Kabwe
Leo Kiongozi wa Chama cha ACT Wazalendo, ndugu Kabwe Z. Ruyagwa Zitto aliripoti Kituo cha Polisi Kamata jijini Dar es salaam kama alivyotakiwa awali na jeshi hilo. Jeshi la Polisi limechukua simu ya ndugu Zitto kwa maelezo kuwa itasaidia uchunguzi wao, na wameahidi kuwa watairudisha kwake kesho jioni, na ametakiwa kurudi kituoni hapo Novemba 21, 2017.

Pia Jeshi la Polisi limetoa taarifa kuwa litakwenda katika Ofisi za Makao Makuu ya Chama cha ACT Wazalendo, kwa Lengo la kufanya upekuzi wa Ofisi hizo wakitafuta nyaraka zilizotumika na Chama kufanya Uchambuzi wa Takwimu za Serikali ambao unaonyesha Uchumi wa Nchi yetu "UNASINYAA".

Ado Shaibu
Katibu - Itikadi, Uenezi na Mawasiliano ya Umma
ACT Wazalendo
Novemba 7, 2017
Dar es salaam
Tags

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Si bora ilivyocjukuliwa...!!!
    Hizi simu za Kichina walishatahadharishwa ...baso tu anayo.
    mwambue anunue Techno bei poa au Nokia Fkash ( kamata mwizi)
    kwani ile yake ilikuwa na Jina

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad