Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Amosi Makalla amekanusha taarifa ambayo imeenea mitandaoni iliyonukuliwa akisema kwamba anategemea kumuandikia barua Rais Magufuli kwa kitendo cha Mkoa wa Mbeya kukosa ushindi kwenye uchaguzi wa Jumapili iliyopita.
Mh. Makalla amekanusha taarifa hiyo wakati akaizungumza na eatv.tv na kusema kwamba kauli yake ilinukuliwa vibaya kwani yeye alitoa kauli hiyo akiwaambia CCM Mkoa wa Mbeya inabidi kuandika barua lakini pia wafanye kujitathmini.
"Unajua nimenukuliwa vibaya. Mimi nilichowaasa wajumbe wa mkutano na wana-ccm watafakari kwanini Chama Cha Mapinduzi kimeshindwa katika uchaguzi kata ya Ibighi. Pia nilisema CCM mkoa wa Mbeya kifanye tathmini kwanini mikoa mingine wamefanikiwa kushinda na Mbeya kushindwa kata kata ya Ibighi nikashauri Chama kifanye tathmini ngazi ya kata , wilaya na mkoa kujua tatizo ni nini.
Hata hivyo Mh. Makalla ameongeza kwamba Ni kwa ajili hiyo nikashauri Chama cha mapinduzi mkoa wa Mbeya wamuombe radhi mwenyekiti wa Ccm Taifa kwa kupoteza kata hiyo. Mimi sikuhaidi kuandika barua ya kuomba radhi na habari zichukuliwe ni za uongo na uzushi.
Hata hivyo Mkuu huyo wa Mkoa amesema kauli yake hyo hata Naibu Spika , Mh. Tulia Ackson naye alikiri ndani ya Mkoa wa Mbeya CCM ni dhaifu hivyo wanapaswa kufanya tathmini upya.