Anthony Joshua Aongoza Tuzo ya Mwanamichezo Bora wa Mwaka 2017 Nchini Uingereza

Anthony Joshua Aongoza Tuzo ya Mwanamichezo Bora wa Mwaka 2017 Nchini Uingereza
Bingwa wa uzito wa juu duniani, Anthony Joshua anaongoza katika orodha ya wachezaji 12 waliyotangazwa kuwania tuzo ya mwanamichezo bora wa mwaka 2017 nchini Uingereza kupitia shirika la BBC.

Joshua mwenye umri wa miaka 28, ambae ni bingwa wazamani wa Olympic na bingwa wa uzito wa juu amekuwa akipendwa zaidi tangu alipotwaa taji lake la WBA na IBO baada ya kumshinda mpinzani wake Wladimir Klitschko katika dimba la Wembley mwezi Aprili.

Huku bondia huyo akifanikiwa kuutetea mkanda wake wa IBF katika pambano lake la hivi karibuni dhidi ya Carlos Takam mwezi Oktoba katika Uwanja wa Cardiff Principality uliyojaza mashabiki 80,000.

Anthony Joshua anakabiliana na ushindani mkubwa kutoka kwa bingwa wa mwaka  2014, Lewis Hamilton ambae pia ni mshindi mara nne wa mashindano ya Formula One mwezi uliyopita na Chris Froome mshindi mara nne wa mashindano ya Tour de France.

Mwanariadha, Mo Farah mshindi wa mbio za dunia mita 10,000 jijini London huku katika listi hiyo akiwemo mchezaji wa Tottenham, Harry Kane.

Kane ni mfungaji bora wa ligi ya Uingereza mwaka 2016/17 na kuisaidia Uingereza kufuzu michuano ya kombe la dunia.

Mchezaji tenis namba moja kwa ubora nchini Uingereza, Johanna Konta nimiongoni mwa wachezaji waliyotangazwa katika listi ya kuwania kinyang’anyiro hicho.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad