BAADA ya mastaa wawili wa filamu Bongo, Aunt Ezekiel na Ester Kiama kuwa kwenye bifu la muda mrefu ambalo hawakuwahi kuweka wazi chanzo chake, hatimaye wamemaliza tofauti zao.
Chanzo makini kililieleza Risasi Jumamosi kuwa mastaa hao kwa sasa ushosti wao umerudi kama zamani na wamemaliza bifu lao ambalo limedumu kwa muda mrefu tangu mwaka jana licha ya kwamba hawajawahi kusema chanzo ni nini ila habari zinadai kwamba ni maneno ya uchonganishi baina yao.
Alipoulizwa Ester alikiri kwamba ni kweli wamepatana, waliamua wao wenyewe kumaliza tofauti zao na siku nyingi tu urafiki umerudi kama kawa.
STORI: GLADNESS MALLY
Aunt Ezekiel na Ester Kiama Wapatana..Hakuna Tena Bifu...Je Wema Sepetu?
0
November 04, 2017
Tags