Baada ya hukumu Lulu, Mama Kanumba afunguka


Mama wa Muigizaji Marehemu Steven Kanumba, Flora Mtegoa amefunguka na kusema kwamba leo atakwenda makaburi ya kinondonni alipoziikwa mwanaye ili kwenda kumzika upya.

Mama Kanumba
Mama Kanumba ametoa kauli hiyo muda mfupi baada ya Mahakama Kuu kumhukumu kifungo cha miaka miwili Muigizaji Elizabeth Michael ambaye alikuwa mtuhumiwa katika kesi ya mauaji bila kukusudia yaliyopelekea kifo cha muigizaji huyo.
"Kwa sasa sina la kusema ila  naishukuru sana Mahakama kwa kutenda haki, pia niishukuru sana Serikali yangu lakini pia nikitoka hapa nitakwenda makaburini kwa ajili ya kumzika upya mwanangu Kanumba". Mama Kanumba
Kwa upande wa Wakili wa Muigizaji Lulu Peter Kibatala ameweka wazi kwamba watakata rufaa kufuatia hukumu ya Mahakama iliyotolewa leo kwa mteja wake.
Muigizaji Lulu leo amehukumiwa kifungo cha miaka miwili jela baada ya kukutwa na hatia ya kumuua muigizaji mwenzake ambaye pia alikuwa mpenzi wake Steven Kanumba usiku wa Aprili 7 2012.
Tags

Post a Comment

2 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. kweli inauma lakini wakati wa kanumba ulikuwa umeshafika hio ilikuwa ni sababu tu yeye mama kanumba ni mtu mzima lulu ni mdogo sana kwa kanumba wangemsamehe tu cos hata luku akiwa jela kanumba harudi

    ReplyDelete
  2. Inauma lakini hata mama inakubidi uone ukweli wa maidha ya mwanao na mazingira ya kifo chenyewe na afya ya mwanao.Lulu hana kosa. Akiwa bado mwenye umri mdogo, alipoteza utoto wake kuwekwa kinyumba na hii di sawa.
    Nakupa pole, lskini kumfunga Lulu si majibu mazuri na di ys kufurahia. aachiwe huru.

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad