Baada ya Kauli ya Haji Manara TFF Yaitumia Timu ya Simba Barua

Baada ya Kauli ya Haji Manara TFF Yaitumia Timu ya Simba Barua
Shirikisho la Soka Tanzania Tff limetuma Barua kwa Klabu ya Simba Sc baada ya kauli ya Afisa Habari na mawasiliano wa Klabu hiyo Haji Manara ambazo kwa Mujibu wa Tff ni tuhuma dhidi ya Waamuzi.

Manara aliitisha Mkutano na Waandishi wa Habari siku ya Jana katika makkao makuu ya Klabu hiyo yaliyopo Msimbazi jijini Dar es salaam, Manara alizungumzia masuala mbalimbali ikiwemo suala la Mwamuzi aliyechezesha pambano kati ya Simba na Yanga siku ya Jumamosi ambapo kwa mujibu wa Manara alikuwa na Makosa mengi ikiwemo kuwanyima penati Simba.

Afisa habari wa Shirikisho la soka Tanzania Alfred Lucas Mapunda amezungumza na waandishi wa kueleza kuwa tayari shirikisho hilo limetuma barua kwa Simba kutaka kujua kusudio lao huku pia wakihitaji Maelezo ya kina kutoka kwa Haji Manara nini lengo lake kutoa kauli hizo ambazo TFF inaona ni uchochezi na uvunjifu wa sheria.
Tags

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Bila ya shaka lengo la Manara ni kutaka haki itendeke kutokana na ushahidi wa video alionao.

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad