Bahati ya Kuolewa Ninayo Ila kwa Sasa Bado Nakula Ujana- Ericah

Bahati ya Kuolewa Ninayo Ila kwa Sasa Bado Nakula Ujana- Ericah
MUUZA nyago kwenye video za wasanii mbalimbali Bongo, Ericah amesema hataki kuolewa kwa sasa, kwa sababu muda wake wa kufanya hivyo haujafika kwani hajamaliza starehe za ujana.

Akipiga stori na Risasi Vibes, Ericah alisema zaidi ya wanaume watatu walishamtolea barua ili wamuoe lakini aliwatolea nje sababu bado anataka aendelee kufaidi ujana wake, kwa kuamini ndoa itambana maisha yake ya kula bata, kwani atakuwa chini ya maamuzi ya mtu mwingine.
 
“Namshukuru Mungu bahati ya kuolewa ninayo, lakini kichwani mwangu siwazi hilo hata kidogo maana kila kwa wakati, naona muda wangu bado, siwezi nikajifosi kufanya kitu ambacho nafsi yangu haijaridhia, nikaenda kumpasua kichwa atakayenioa,” alisema
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad