Bodi Itafungua Dirisha la Kukata Rufaa kwa Wanafunzi Waliokosa Mikopo- Badru

Bodi Itafungua Dirisha la Kukata Rufaa kwa Wanafunzi Waliokosa Mikopo- Badru
Mkurugenzi wa Bodi ya mikopo ya elimu ya juu (HESLB), Abdul Razaq Badru amesema bodi hiyo itafungua dirisha la kukata rufaa kwa wanafunzi waliokosa mikopo.

Badru ameyasema hayo leo wakati akifafanua vigezo na sifa za mwanafunzi kupata mkopo baada ya kuwepo kwa kasoro kadhaa kwa baadhi ya waombaji katika awamu ya kwanza ya wanafunzi wa mwaka wa kwanza.
“Kwa wale wenye changamoto ndogondogo labda walikosea, tutatangaza dirisha la kukata rufaa mapema wiki ijayo na tutashughulikia watakaokamilisha vigezo watapata mkopo lakini wanatakiwa kuzingatia maelekezo tutakayoyatoa”, ameongeza.

“Waombaji wanatakiwa kuwa makini na kufuata maelekezo kwa mfano unakuta mtu anasema yeye ni Yatima lakini hajaambatanisha uthibitisho wowote wa wazazi wake kufariki au mwingine anasema ni Mlemavu lakini hana udhibitisho wowote kwahiyo huwezi kumpa mkopo kwasababu hana sifa”, amesema Badru.
Aidha mkurugenzi amesema katika majina ya waombaji waliyoyapokea na kudhibitishwa na TCU kwamba yamepata vyuo na wakayapitia wakajiridhisha hayana kasoro kwenye uombaji, tayari wanafunzi 29,578 wameshapata mkopo na wameanza masomo ambapo kiasi cha shilingi bilioni 96 zimetumwa vyuoni.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad