Mkurugenzi mtendaji wa bodi hiyo Boniface Wambura amesema Simba imeonywa kwa kosa la kumsimamisha kwenye benchi la ufundi kocha wao msaidizi Masoud Juma raia wa Rwanda kwenye mchezo wao na Njombe Mji bila kuwa na vibali vya kufanya kazi nchini.
Mbali na onyo hilo klabu ya Simba imeadhibiwa kwa kupigwa faini ya Tsh. 300,000 kwa kosa la kuchelewesha kuwasilisha orodha ya majina ya wachezaji waliocheza mchezo wa siku hiyo. Wambura amesema Simba waliwasilisha majina saa 9:00 mchana ikiwa ni saa moja kabla ya mchezo kitu ambacho ni kinyume na kanuni.
Aidha Wambura amesema kikao cha bodi ya ligi bado kinaendelea kujadili mambo mbalimbali yanayohusu ligi kuu pamoja na ligi daraja la kwanza na daraja la pili ambapo baadhi ya dosari wamezipeleka kwenye kamati ya nidhamu kwaajili ya hatua zaidi.