- Mahakama ya Juu nchini Kenya imetupilia mbali kesi zilizofunguliwa na wafuasi wa NASA za kupinga ushindi wa Urais wa Uhuru Kenyatta, kwenye uchaguzi wa marudio wa Oktoba 26, 2017
- Kesi hiyo ambayo ilikuwa moja kwa moja kwenye vyombo vya habari, iliongozwa na majaji 6 akiwemo Jaji Mkuu David Maraga, na kutoa uamuzi kuwa Uhuru Kenyatta ni mshindi halali wa uchaguzi wa Oktoba 26.
- Kufuatia uamuzi huo wa mahakama ya Juu nchini Kenya, Uhuru Kenyatta anatarajiwa kuapishwa wiki ijayo, na kuwa Rais wa Jamhuri ya Kenya kwa muhula wa pili.
- Ikumbukwe uchaguzi wa marudio ulifanyika baada ya Mahakama ya Juu kufuta matokeo ya Urais ya uchaguzi wa kwanza wa Agosti 8, 2017 na kutaka urudiwe mara ya pili.