Brigty Akataa Kufananishwa na Belle 9 "Kunatofauti Kubwa Kati ya Mimi Naye Nilianza Kuingia Studio Kabla Yake"

Brigty Akataa Kufananishwa na Belle 9 "Kunatofauti Kubwa Kati ya Mimi Naye Nilianza Kuingia Studio Kabla Yake"
Msanii wa Muziki Bongo Bright amesema kuna utofauti mkubwa kati yake na Belle 9.

Muimbaji huyo ambaye kwa sasa anafanya vizuri ngoma ‘Ni Wewe’ ameiambia XXL ya Clouds Fm kuwa wapo wanaowafanisha lakini kiuhalisia hawafanani na walishafanya hata ngoma pamoja ili mashabiki kuona utofauti wao.

“Hapana, mimi nimeingia studio kwa mara kwanza mwaka 2006 sidhani kama Belle 9 alikuwa amefahamika lakini kutokana amefahamika na mimi nimekuja kufahamika baadaye yeye ameshapata nafasi lazima mtu awe anaongea hivyo” amesema Bright.

Ameongeza kuwa kutokana na watu kuwafananisha ndio sababu ya kufanya kazi kwenye menejiment moja kipindi cha nyuma ambapo hata uongozi wao ulikuwa unawafanisha lakini kila mmoja ana kitu chake.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad