CCM Arusha yampa ushauri wa bure Godbless Lema

Chama cha mapinduzi (CCM) Arusha kupitia kwa katibu Elias Mpanda kimefunguka kuhusu Wafuasi wanaodaiwa kuwa wa CHADEMA kuwashambulia watu watatu wa CCM akiwemo Mgombea Udiwani kata ya murieti Fransis Mbise.

Mpanda amesema “Sisi CCM kwakweli ni Wastaarabu na ninataka niwahakikishie kati ya kata zote 8 ambazo nimesema tutashinda, tutashinda kwasababu tuna hoja za kusema juu ya Wananchi“

“Nashukuru Wananchi wa Arusha na kama sio Tanzania nzima wameshatambua dhamira kubwa ya CHADEMA kwamba dhamira yao sio kuwaletea Wananchi maendeleo bali kuwatumia kwa maslahi yao binafsi”

“Ushauri wa bure kwa ndugu Godbless Lema, kwanza Wafuasi wa CHADEMA niwaombe sana wasitumike vibaya kwasababu hata jana walioleta fujo wote walikamatwa na wako polisi lakini Godbless alikimbia pamoja na katibu wa chama wa Wilaya”
Tags

Post a Comment

3 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Ccm kama chama tawala. Mnamtumia raisi kwa manufaa yenu kichama. Ukweli ni kwamba, mtamtumia raisi kwa muda tu. Kununua watu, kutoa rushwa, kutoruhusu katiba ya wananchi, kutokuuona ubivu wa viongozi wenu na wanachama wenu. Mnaona mabaya yao tu mara wanapoondoka kujiunga na chadema ndipo wanageuka kuwa uozo. Mnafichiana ukweli, hampo wa kwrli wala hampo kwa manufaa ya wananchi. Mnatumia chama, na serikali pamoja na kuviita hivi vyote ni ccm. Mtawapata wale wapumbavu wasio wasomi, wasiojua kufikiri, mnaowafunga midomo, wale waogo, wataka vyeo, badala ya kutoa elimu na kumwelimisha mtanzania mbazidi kumweka na kumwingiza mtanzania kwenyevujinga zaidi. Nilifikiri chini ya uongozi wa ndugu Magufuli mtabadilika, la hasha. Mnazidi kutumia uwingi wenu kuwaogopesha watanzania wasiamke na kuwa huru na kudai maendeleo yao ya kweli na binafsi. Badala yake mbatoa kitu fulani . Ingawa ni serikali inayotoa ambayo ni kodi zao mbageuza na kuwaambia watanzania ni ccm inafanya hivin
    Vi. Ni wajinga tu wasio na elimu na mwamko safi na wenye nfinyo kifikra ndio mtawaokota. Matokeo haya ni maendeleo bandia mnayaweka na si maendeleo ya mtu binafsi yanayomeongezea kipato mtanzania wa kawaida. Siasa chafu na mbovu ndo hizi. Na ni mbaya sana kwa taifa letu. Tunapopata mwanya kwenda mbele wanajitokeza viongozi wachafu wakiwaogopesha wananchi na kuiingiza nchi nyuma zaidi. CCM kamwr haitaweza na imeshindwa kumthamini mtanzania. CCM bado haijawa kweli. CCM bado na mifumo ileile, uwongo, uoga, kulindanda, maneno matupu, hakuna hadhi , woga, utu, unadhifu, ukweli ni kubotonga kimaneno tu. Je lini watanzania wataamka kielimu na kutokurugusu kudanganywa na watu wachache. Lini watu mtaanza kutumia akili zenu badala ya kulimbikizwa na oungo wa kichama, lini watanzania mtaamka na kudai maendeleo yenu mnayoyataka, lini watanzania mtaamka na kudai uhuru wa kutoa ya ndani yanayowasibu. Lini mtakuwa huru kumwambia raisi tunakuunga mkono tu ukituruhusu sisi tuliokuchagua utusikilize , utujali na ufanye au wote kwa pamoja kimakubaliano na heshima tulijenge taifa letu na si utakavyo wewe bali wengi wetu. Mnamlipa. Mue mnauhuru huu. Lini chama kitalazimishwa kujutambua ni tanzania kwanza na mipango ya tanzania chama tawala kiheshimu na kitekeleze matakwa ya watu? Lini wanaccm itabidi wajue tofauti ya chama na serikal?

    ReplyDelete
  2. Wakati wa Mubgu ukifika hakika kila mtu ataiona chadem madarkani hakuna kukata tamaaa

    ReplyDelete
    Replies
    1. tehe tehe tehe! Huo wakati wa Mubgu mpaka ukifika hiyo chadem sijui kama itakuwepo madarkani.....du mwandishi anajazba hatari, sio kwa 'michapio' hiyo hahahaha

      Delete

Top Post Ad

Below Post Ad