Chadema Hakiwezi Kutetereka au Kufa Kwasababu ya Katambi Kuondoka

Chadema Hakiwezi Kutetereka au Kufa Kwasababu ya Katambi Kuondoka
Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe amesema chama hicho hakiwezi kutetereka au kufa kwa kiongozi au mwanachama wake kuondoka.

Amesema kuna mkakati mkubwa unaotumia fedha unaofanywa kuwalaghai viongozi na wanachama wake kukihama chama hicho.

Kauli hiyo ameitoa leo Jumatano baada ya aliyekuwa mwenyekiti wa vijana wa chama hicho, Patrobas Katambi kutangaza kujiunga na CCM.

Akizungumza leo Jumatano na Mwananchi, Mbowe ambaye pia ni amesema, "Tuko ‘strong enough’ sio mara ya kwanza watu kuondoka hivyo wanachama wetu wasiogope waendelee kujenga chama na kuendelea na kampeni za udiwani,"

"Huiwezi kututeteresha, kuondoka kwa Katambi si hivi hivi, ushawishi wa fedha umetumika...ingawa ni haki yao ila hao hawaondoki kwa mapenzi yao na hilo halina ubishi,"

"Badala ya nguvu na fedha kuzielekeza kujenga viwanda wao nguvu wamezielekeza kushawishi viongozi wetu, wamewashawishi wengi na Katambi ni miongoni ingawa wengine wamekataa."

Mbowe amesema, "Katambi alikuwa katika majukumu ya chama na aliwaaga wenzake anakwenda kumuguza mama yake mgonjwa hivyo akakatiwa tiketi ya ndege, kumbe alikuwa anakwenda kukamilisha dili ambalo naambiwa limetumia saa 48 kukamilika."

Amesema Chadema ilipofika haiwezi kufa kwani imejijenga na hapo walioondoka lakini mpaka sasa kimeendelea kuwapo.

Mbowe amesema mwitikio wa wananchi katika kampeni za udiwani kwenye kata 43 umeishtua CCM ikiwamo kuhama kwa aliyekuwa mbunge wa Singida Kaskazini, Lazaro Nyalandu.

Post a Comment

5 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Pole sana Mbowe, ninyi kila anaeondoka chama chenu shurti mseme alipewa fedha au hakuwa anasaidia kitu, ndo siasa hizo.

    ReplyDelete
  2. hahahaha!Macho yako pamoja na maneno yako vyote havina ushirikiano kwa uongo ulivyokuzidi....wale walohamia kwenu mliwapa 'PAPA'.......mfyuuuuu maneno ya mkosaji.....NA BADO!!

    ReplyDelete
  3. Mbowe Povu la nini....!!!!
    Mie nasikia wewe ni mwendesha chama kidikiteta. Je ni Kweli?
    Manake Zitto ulimfanyiaga halafu ukamfukuza...!!!
    Hawa ndugu zetu wameshindwa kuona Kila Juhudi mnabeza na ukweli unaonekana.
    Sasa hawa ni Viongozi na ni Wazalendo....!!! Wanataka kuitumikia nchi hii kwa Hali na Mali na Afya zao.. na wameamua kuunga mkono na ushirikiano na jembe la Awamu ni ya Tano.
    Karibuni sana mmerudi nyumbani.
    Tanzania ni yenu na CCM ni chama chenu. Cha muhimu ni kwamba tunaijenga Tanzania kwa Watanzani.

    ReplyDelete
  4. TUTAKUPELEKA KUNAPO HUSIKA KWA HII KAULI YA "DILI IMECHUKUA SAA 48" LAKIMA UIJIBU

    ReplyDelete
  5. Kabisa sioni sababu TAKUKURU kukaa kimya kwa hii kauli ya Mbowe anayodai kuna RUSHWA imetumika kwa hawa watanzania wenzetu walioamua kukimbia kutoka Chadema baada ya kugundua ni Chama cha hovyo. Kwa tuhuma anazotoa Mbowe ni nzito tunaomba mamlaka husika imuamuru muheshimiwa Mbowe kuthibitisha madai yake ili kuondoa sitofahamu kwa watanzania .

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad