Chadema Yabariki Uamuzi wa Aliyekuwa Mwenyekiti Wao wa Bavicha

Chadema Yabariki Uamuzi wa Aliyekuwa Mwenyekiti Wao wa Bavicha
Katibu Mkuu wa Chadema, Dk Vincent Mashinji amesema chama hakina mgogoro na aliyekuwa Mwenyekiti wa Bavicha, Patrobas Katambi ambaye ametangaza kujiunga na CCM kwa kuwa ni haki ya Kikatiba.

Akizungumza na Mwananchi leo Jumanne baada ya Katambi kuhamia CCM, Dk Mashinji, “sisi kama chama msimamo wetu tuliuweka tangu madiwani walivyoanza kuondoka, tukaweka msimamo wazi kwamba, suala la mtu kuondoka kwenye chama au kubaki ni suala la Katiba ya nchi ambayo inampa mtu uhuru wa kuhama na kwenda kwenye chama anachotakana.”

Amesema kuwa haoni sababu ya kumzuia mtu kuondoka kwa kuwa mtu anapoamua kwenda sehemu yoyote anakuwa na matarajio.

Pia, Dk Mashinji amesema anamtakia heri (Katambi) na kuwataka CCM kumtumia katika sehemu ambavyo wanaona anafaa kutumika kwa faida ya Watanzania wote.

Soma: Katambi asema yuko tayari kuitwa msaliti

“Hatuna mgogoro wowote na kimsingi mimi nimtakie tu heri (Katambi) na wakipenda (CCM) wamtumie kwenye eneo watakaloona anafaa kutumika kwa faida ya Watanzania wote,” amesema

Hata Hivyo, Dk Mashinji amesema kuwa walikuwa wanamuandaa Katambi asaidie chama hicho kwenye kitengo cha sheria.

“Alikuwa anamalizia masomo yake ili awe wakili na tulikuwa tumeshaanza kumuandaa ili atusaidie kwenye kitengo cha sheria ndani ya chama,”

Katambi ametangaza leo kujiunga na CCM mbele ya Mkutano wa Halmashauri Kuu ya CCM (NEC) unaofanyika katika Ukumbi wa Ikulu jijini Dar es Salaam.
Tags

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. WAPI NASARI.....NA HUYO NAE VEPE??? KAPEWA RUSHWA NA MKUU WA WILAYA GANI.......KINO, TMK AMA.....HAHAHA TAKUKURU HAWAHUSIKI HAPO KWELI....HAHAHAHA MTAISOMA-NAMBA KABLA 2020....HAPA-KAZI-TU, MAJUNGU HUKO KWENU TEHETEHETEHE

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad