Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema amesema kuwa kitu cha msingi ambacho wananchi wanatakiwa wajue ni kwamba Chama cha Mapinduzi (CCM) kimefika mwisho huku akisema mshahara wa dhambi ni mauti na Chama hicho kina dhambi kubwa sana iliyokaribia mauti.
Lema ameyasema hayo Jumapili hii katika uwanja wa Shule ya Msingi Mhandu mkoani Mwanza ambako Mbowe alikuwa anahutubia mkutano wa hadhara wa kampeni za udiwani katika uchaguzi mdogo utakaofanyika Novemba 26,2017.
“Tundu Lissu yuko hospitali ana uguza majeraha ya risasi si kwasababu alifumaniwa, si kwasababu ni mwizi ni kwasababu ya kupigani haki zenu, dhambi kubwa kuliko dhambi zote duniani ni uoga na sasa kitu cha msingi sana mjue tu kwamba CCM imefika mwisho. Mmesikia Zimbabwe waliompindua Rais Mugabe sio Wapinzani aliokuwa ana wapiga mabomu ni Wanajeshi aliwavalisha yeye vyeo, walewale machinga waliokuwa wanamshangilia Mugabe leo wameandamana kusema Mugabe toka, nitamshukuru Mungu sana siku nikiona hiyo siku inafika mahali hapa, mshahara wa dhambi ni mauti na dhambi ya CCM ni kubwa sana imekaribia kwenye mauti kwasababu leo yupo Mwenyekiti wetu hapa na Katibu wetu Mkuu yuko mahali hapa na Lazaro Nyalandu yuko hapa,” alisema Lema.
“Ila niwaombe watu wa Kata hii, ukiibiwa kura unaenda nyumbani mwanaume una mwambia mke wako tumeibiwa kura mama mtafutie sketi huyo baba kama ambavyo Katiba inaruhusu kuzuia uhalifu wa aina yoyote kwa mwananchi yoyote ndivyo ambavyo Katiba ina ruhusu kulinda kura zako viongozi wameandaa mawakala wazuri sana kwahiyo ukishaa piga kura kaa mita 100.”