Chama cha Zanu- PF Kumbuluza Mahakamani Mugabe

Chama cha Zanu- PF Kumbuluza Mahakamani Mugabe
Mtandao wa Twitter unaofuatilia taarifa za vyombo vya habari nchini Zimbabwe unaripoti kuwa Kiongozi wa chama tawala Cha ZANU PF anaamini mchakato wa kumshtaki Bwana Mugabe utaendelea kama ilivyopangwa Jumanne , wakati ambapo chama bunge linatarajiwa kukaa.

Hii ni kama muda wa makataa uliowekwa wa kujiuzulu kwake ambao ni Jumatatu saa sita adhuhuri utakwisha kabla Bwana Mugabe hajajiuzulu.
Mamlaka ya Mugabe yalidhoofishwa tangu jeshi lilipoingilia kati Jumatano, wakati ulipoibuka mzozo juu ya nani anayepaswa kumrithi .

Mzozo huo uliibuka wiki mbili zilizopita wakati kiongozi huyo mwenye umri wa miaka 93- alipomfuta kazi makamu wake Emmerson Mnangagwa, jambo lililowakasirisha makamanda wa kijeshi walioona kuwa ni jaribio la mkewe Grace kutaka kuwa rais.
Halikuwa tangazo ambalo baadhi ya waZimbabwe walilisubiri. Bwana Mugabe bado ni rais na haijawa wazi ikiwa bunge sasa litaanza mchakato wa kumshitaki.

Watu wa Zimbabwe walikuwa wanatarajia kusikia mugabe akijiuzulu kulingana na madai yao.
Baadhi ya wale waliokusanyika kufuatilia hotuba yake kwenye vilabu waliiambia BBC kuwa wamekatishwa tamaa na kutojiuzulu kwa rais Mugabe.
Hata hivyo hali ya imeendelea kuwa tulivu katika maeneo mengi ya Zimbabwe, huku wengi waliendelea kusubiri mchakato utakaofuata.

Duru kutoka ndani ya mazungumzo ya hatma ya Mugabe zimeiambia BBC kuwa Mugabe mwenye umri wa miaka 93 alikuwa amekubali kuondoka madarakani , lakini baadae akabadili mawazo yake
Jeshi linatarajiwa kuwa na mkutano na waandishi wa habari Jumatatu asubuhi pamoja na Muungano wa Wapiganaji waliopigania Uhuru wa Zimbabwe.

Katika hotuba yake ya kwanza kwa taifa tangu jeshi lichukue madaraka Jumatano, Mugabe hakujiuzulu na alisema kuwa ameazimia kuongoza kongamano lijalo la Zanu-PF.
Hatma yake sasa iko mashakani kwani kulingana na mbunge wa Zanu-PF Terence Mukupe anasema kongamano hilo ni mahala panopofaa kumuidhinisha kiongozi mpya anayependelewa na chama cha Zanu-PF

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad