DC Hapi Aapa Kuchuana na Halima Mdee Kawe 2020...Adai Lazima Amng'oe


Mkuu wa Wilaya Kinondoni, Ally Hapi ameahidi kumng’oa Mbunge wa Kawe, Halima Mdee katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2020.

Hapi alisema hakuna haja ya kuacha jimbo hilo la Kawe na majimbo mengine katika wilaya hiyo kuendelea kuwa chini ya upinzani kwa kuwa wananchi wana imani na CCM.

Kauli Hiyo aliitoa Dar es Salaam jana katika Kata ya Mbweni ambako CCM iliibuka na ushindi katika uchaguzi huo wa udiwani.

Alisema kutokana na matokeo ya uchaguzi kata ya Mbweni Hashim Mbonde (CCM) aliibuka kidedea kwa kura 2049 dhidi ya Chadema kura 1,093.

Alisema hizo ni salamu kwa Mdee kuwa mwaka 2020 atafute kazi nyingine na si ubunge katika jimbo hilo. “CCM mpya haina makundi, wanaoshindwa na kushinda wote ni kitu kimoja na wale wanaokwepa falsafa za chama watakaa pembeni,” alisema Hapi.

Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Kinondoni , Alord Maluma, alisema ushindi wa Mbonde ni wa CCM na atahakikisha Kinondoni inarudisha uhusiano na uhusiano mwema wa wanachama na wannachi ili kukomboa kata, mitaa na majimbo.

Katika uchaguzi huo, CCM ilishinda kwa kupata kura 2049 Chadema 1093, CUF 114 na SAU kura 12.
Tags

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Huyu lazima aondoke 2020.
    Ali Hapi.... lazima tuwajulishe wananchi ukweli halisi ws hawa watovu wa Nidhamu.
    na kama hajaolewa tuwape waume ili siku moja waweze kutuimarishia taifa kwa uzazi bora.
    Mtoto mzuri anafaa kuwekwa ndani na kuitwa Mama.
    Halima Dili hiyo... inakuja umuri unakwenda na afya pia.

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad