Deni la Milioni 32.5 Zaiweka Hatarini Hoteli DC Atoa Ziku Saba Kulipa Deni Hilo

Deni la Milioni 32.5 Zaiweka Hatarini Hoteli  DC Atoa Ziku Saba Kulipa Deni Hilo
Mwenyekiti wa kamati ya Ulinzi na usalama wilaya ya Kahama Fadhil Nkurlu ametoa siku saba kwa uongozi wa hoteli ya Mongo kulipa deni la mapato ya serikali shilingi milioni 32.5 na kuwalipa fidia waandishi wa habari walioibiwa vifaa vya kazi wakati wamelala hotelini hapo.

Nkurlu ametoa maagizo hayo leo Ijumaa baada ya kutembelea hoteli hiyo kutokana na uongozi kukaidi agizo la Mamlaka ya Mapato(TRA) la kulipa kiasi hicho kabla au ifikapo Julai 5.

Meneja wa TRA Mkoa wa Kodi wa Kahama, Jacob Mtemang’ombe amethibitisha hoteli hiyo kudaiwa Sh30 milioni inayotokana na kodi ya asilimia 10 ya mauzo yaliyofanyika zaidi ya mwaka mmoja uliopita.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad