Katibu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Dr. Vicent Mashinji ametupa jiwe gizani na kudai kwamba kitendo cha dola kumkamata mtu kwa tuhuma za uchochezi ni udhaifu wa serikali katika kujibu hoja.
Dr. Mashinji amesema kwamba siasa zenye msamiati wa uchochezi huwa hazipo hivyo kwani wadhaifu huwa ndiyo wanaotumia mabavu na siyo hoja.
Kupitia ukurasa wake wa Twitter Dkt Mashinji ameandika "Najenga hoja, unasema mi mchochezi. Kweli umekosa ushawishi jitafakari upya, siasa za sasa msamiati wa uchochezi haupo. Ni hoja kwa hoja!"
Hivi karibuni viongozi mbalimbali wa upinzani wamekuwa wakikamatwa na jeshi la polisi mara kwa mara kwa tuhuma za uchochezi
Wewe Mashinji Ni Daktali WA magonjwa yepi.
ReplyDeleteManake unatia wasieasi ikiwa Ni mfinyu WA uelewa Na maansiki yako Na mwelekeo wako ndiyo jinsi ulivyo andikika inawalakini.
Je juu udaktali uliumba au ....
Na ukitaka kuonekana tukufate wapi?
Muhimbili au Mirembe?
Huo ndo ufinyu wa mawazo. Kwa nini usimjibu hoja yake badala ya kutafuta udaktari wake? Tanzania ni ya kila mtanzania.kila mtu ana uhuru wa kutoa maoni na mtazamo wake.mambo ya ku shambulia mtu badala ya hoja si sahihi
ReplyDeleteAliyekwambia kuwa daktari ni hadi uwe unatibu watu ni nani? hujui daktari ni daraja mojawapo la taaluma? au ndo ulishazoea kuona waliovaa mavazi meupe na ukaita daktari hata kama ni muuguzi? daktari ni taaluma, ni mtu aliyehimu degree tatu akaitwa daktari hivyo usikariri wa muhimbili na kwingineko. rudi ujibu hoja yake usianze kukosoa huku hujui unachokikosoa.
ReplyDelete