Mnangagwa ametoa kauli hiyo mara baada ya kurejea nchini Zimbabwe akitokea Afrika Kusini ambako alikimbilia baada ya kufukuzwa kazi na aliyekuwa rais wa nchi hiyo Robert Mugabe.
Mnangangwa ametumia nafasi hiyo kuhutubia umati mkubwa uliofika kumlaki katika uwanja wa ndege wa Harare ambapo alisema kwamba anataka kukuza uchumi, amani na ajira.
Inakadiriwa kuwa asilimia 90 ya watu nchini Zimbabwe hawana ajira.
Mnangagwa, anatarajiwa kuapishwa kuwa rais wa nchi hiyo asiku ya ijumaa kulingana na taarifa iliyotolewa na Television ya Taifa. Kufukuzwa kwa kiongozi huyo kulifanya jeshi la nchi hiyo pamoja na chama tawala kuingilia kati na kumaliza utawala wa Mugabe uliodumu kwa miaka 37.
Aidha kiongozi huyo amelishukuru jeshi kwa kuendesha mchakato wa kumuondoa Mugabe kwa amani kwa madai kwamba alishawahi kukabiliana na matukio kadhaa ya kutaka kuuwawa.
Msemaji wa chama tawala cha Zanu-PF amesema Mnangagwa, mwenye umuri wa miaka 71, ataliongoza taifa hilo mpaka mwakani mwezi Septemba utakapo fanyika uchaguzi mkuu nchini humo