Godbless Lema Amshauri Spika Ndugai Kuhusu Wabunge

Mbunge wa Arusha Mjini Godbless Lema amemshauri Spika wa Bunge la Tanzania Mh. Job Ndugai kutumia busara kuwaondoa bungeni wabunge nane walioingia Bungeni kuziba nafasi za wabunge nane waliokuwa wamevuliwa uanachama wa chama cha CUF Julai 24.

Lema aetumia nafasi yake kuandika ujumbe huo ikiwa ni siku moja baada ya Mahakama Kuu kutengua kufukuzwa kwa Wabunge 8 na Madiwani 2 wa Chama cha Wananch CUF mpaka pale shauri la msingi litakaposikilizwa.

Lema kupitia ukurasa wake wa Twitter ameandika   "Mh Spika anapaswa, kuzingatia kwa busara uamuzi uliotolewa na mahakama kwa kuwaondoa wale Wabunge wa Lipumba ndani ya Bunge na kuwarejesha Wabunge halali sasa . Mpaka hapo haki itakaposhinda zaidi"

Wabunge hao nane walivuliwa uanachama Julai 24 Baraza Kuu la Uongozi la Taifa la Chama cha Wananchi, CUF linaloongozwa na Profesa Lipumba  kwa madai ya utovu wa nidhamu, yakiwemo kukisaliti chama hicho.



TAZAMA Video Mpya ya Rosa Ree Ambayo Imekuwa Gumzo Mtaani:

Press Play:

Tags

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Godolesi.. Wewe na Uamuzi wa Mahakama au uendeshaji wa shughuli na Mamlaka ya Bunge.
    Ni wapi na wapi kwa Kilaza Wewe????
    Nyamaza na Uangalie yako.
    Unawashwa washwa nini???
    Ndungai anayaelewa Majukumu yake na anaelewa nini cha kufanya kwa wakati Muafaka.
    Usiingilie na kushauri kazi za Watu.
    Yako yanakushinda. Angalia Mrisho Gambo anataka Maendeleo ya Mkoa wako na Umsaidie ipasavyo Mcheleweshaiwewe kuwa mzalendo. na ufanye kazi na siyo Longo longo....!!!
    Hapa Kazi Tu.

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad