Hamorapa- Ipo Siku Wema Sepetu Atakuwa Wangu Ugumu Alopata Janjaro Umenipa Matumaini

  • Hamorapa- Ipo Siku Wema Sepetu Atakuwa Wangu Ugumu Alopata Janjaro Umenipa Matumaini

Tetesi za rapa Dogo Janja kufunga ndoa na muigizaji, Irene Uwoya zimemfanya rapa Harmorapa kuamini kuwa ndoto yake ya kufunga ndoa na mrembo wa filamu, Wema Sepetu itatimia.

Harmorapa miezi michache iliyopita alijinadi katika mitandao ya kijamii kwamba anampenda Wema Sepetu na angependa kufunga naye ndoa hata hivyo mrembo huyo alisema hawezi kutoka kimapenzi na rapa huyo na anamchukulia kama mdogo wake.

Jumatatu hii baada ya kuona picha za Dogo Janja amefunga ndoa na Irene Uwoya, amedai picha hizo zimemfanya aamini hata yeye siku moja atafunga ndoa na Wema Sepetu.

“Dah naamini sana katika ndoto kuwa ipo siku ndoto inayoota itatimia na kuwa kweli sina cha kusema zaidi ya kumpa hongera Dogo Janja naamini ushupavu na kutovunjika moyo kumemfanya leo akawa mume wa mwanamke wa ndoto zake,” aliandika rapa huyo mtandaoni.

Aliongeza, “Nami sivunji imani naamini Wema Sepetu ipo siku atakua wangu ugumu alioupata Janjaro umenipa matumaini kikubwa ni kutulia na ndoto yangu na kulenga ipo siku itatimia… One day you will be mine….❤ @wemasepetu,”

Baada ya kauli hiyo, Dogo Janja alimpa moyo rapa huyo mwenzake na kumtaka kuwa mvumilivu.


Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad