Hii Hapa Tiba Mbadala ya Ganzi Mikononi, Miguuni

Hii Hapa Tiba Mbadala ya Ganzi Mikononi, Miguuni
GANZI mikononi na miguuni, ni tatizo linaloashiria kukosekana kwa fahamu katika sehemu hizo. Hisia ndiyo inakosekana kwa sababu hakuna damu na neva zinakosa mawasiliano ya moja kwa moja na ubongo.

Ni jambo la kawaida linalowapata watu wengi sana katika miaka ya hivi karibuni, lakini pasipo kujua nini chanzo chake wala tiba.

Vyanzo vya ganzi mwilini

Vifuatavyo vinatajwa kuwa vyanzo vya ganzi mwilini mwa binadamu:

1. Shinikizo la muda mrefu kwenye miguu na mikono.2. Kuwa karibu na vitu vyenye baridi sana kwa kipindi kirefu.3. Mabadiliko ya muda mfupi kwenye neva/mishipa.4. Ajali kwenye neva.5. Kunywa pombe kupita kiasi.6. Uvutaji sigara na bangi.7. Uchovu usioisha.

8. Kutokujishughulisha na mazoezi ya viungo kila mara.9. Ukosefu wa vitamini B12 na Magnesiamu mwilini,10. Ugonjwa wa kisukari n.k

Kwa kawaida, ganzi inayotokea kwa dakika kadhaa na kupotea huwa haina shida yoyote.

Inaelezwa, ni vyema kuonana na daktari mapema, iwapo ina kawaida ya kutokea kila mara na inadumu muda mrefu. Inaweza kuwa ishara ya ugonjwa fulani unaohitaji matibabu ya haraka.

Kuumwa ganzi miguuni na mikononi, kunaweza kuwa jambo linaloudhi sana kwa mgonjwa.

Kuna dawa kadhaa za asili. Hata hivyo, hapa mimi leo nimekuandalia dawa za asili unazoweza kuzitumia kuondokana na tatizo hili.

Matibabu mbadala mwilini:

1. Massaji; Kufanya mazoezi ya massaji wakati unapopatwa na ganzi ni namna nzuri ya kutibu ganzi.

Massaji inaongeza msukumo na mzunguko wa damu jambo ambalo mwisho ni tiba kwa tatizo la ganzi. Zaidi masaji inasaidia kusisimua neva na misuli na hivyo kuimarisha na kuongeza mzunguko wa damu kwa ujumla.

*Kwa matokeo ya uhakika weka mafuta ya nazi au ya zeituni au ya mharadali (mustard oil) kwenye viganja vya mikono yako .

*Pakaa sehemu unapopata ganzi

*Massaji maeneo hayo na mikono yako kwa wastani wa dakika tano mpaka saba.

*Fanya mara tatu hata tano kwa siku.

2. Mazoezi ya viungo; Hayo husaidia kuimarisha mzunguko wa damu na kuongeza oksijeni katika sehemu zote mwilini, hivyo kuzuia kupata ganzi.

Mazoezi ndiyo namna pekee ya bure ya kujikinga na kujitibu na magonjwa mengi ikiwamo tatizo la mwili kupatwa na ganzi.

Mazoezi maalum; hapo inajumuisha kulala chali, kunyoosha mikono chini. Kisha nyanyua mguu mmoja juu unyooke, shusha chini mguu na unyanyue wa pili hivyo hivyo juu kisha chini. Endelea hivyo hivyo kwa mara kumi kumi kwa mizunguko mitano, zoezi lichukue wastani wa dakika 10

Kisha, anyanyuke na ajipigie saluti mwenyewe, akianzia mkono wa kulia mara 15, kisha unahamia mkono wa kushoto mara 15 tena mizunguko mitano.

Hatua inayofuata ni; simama,- chuchumaa, simama, chuchumaa, simama, hivyo hivyo mara 15 kwa mizunguko mitano.

Pia, unasimama wima, nyoosha mikono yote juu na uishushe mabegani. Hivyo, mikono juu na kisha mikono mabegani mara 15 kwa mizunguko mitano.

Fanya hivi mara nne mpaka tano kwa wiki. Mazoezi ya kukimbia, kuendesha baiskeli, kuogelea ni mazuri pia.

3. Bizari; Bizari au manjano inayojulikana kwa Kiingereza kama ‘Turmeric’ ina kitu muhimu ndani yake kijulikanacho kama ‘curcumin’ kinachosaidia kuongeza msukumo wa damu katika sehemu zote ya mwili.

Pamoja na hayo, bizari inasaidia kuondoa maumivu na hali ya kutojisikia vizuri mwilini.

Kinachofuata ni kuongeza kijiko kidogo kimoja cha chai cha unga wa bizari ndani ya kikombe cha maziwa ya vuguvugu, ongeza kiasi kidogo cha asali na unywe kutwa mara moja;

Mtu anaweza kutengeneza uji mzito (paste) wa bizari na maji na utumie kufanya massaji sehemu unapopata ganzi.

4. Mdalasini; Mdalasini ina kemikali na viinilishe mbalimbali, ikiwamo manganizi na potasiamu na vitamini nyingi za kundi B.

Faida zake za kiafya zinajumuisha kuongeza msukumo wa damu kwenye miguu na mikono yako na hivyo kusaidia kutibu tatizo la ganzi.

Wataalamu wa tiba asili wanashauri gramu mbili mpaka nne za unga wa mdalasini, zitumike kila siku kwa ajili ya kuhamasisha, mzunguko mzuri wa damu mwilini.

Changanya kijiko kidogo kimoja cha chai ya mdalasini ya unga katika glasi ya maji ya moto na unywe yote mara moja kwa siku.

Au changanya kijiko kimoja kidogo cha chai cha mdalasini ya unga na kijiko kidogo kingine cha asali na ulambe mchanganyiko huo kila siku asubuhi, kwa wiki kadhaa.

Angalizo la mdalasini feki; Ni muhimu sana kuelewea kuhusu mdalasini hasa ambao hutumika kama dawa.

Siyo kila mdalasini unaouona unaweza kukupa maajabu haya, mwingine ni sumu kabisa mwilini. Na watu wengi hawajui hili jambo.

(a) Ceylon cinnamon

Mdalasini ambao hutumika kama dawa hujulikana kwa kitaalamu kama ‘Ceylon cinnamon’ na kwa kawaida wenyewe huuzwa gharama sana.

Kwa kawaida zina ladha tamu na harufu ya kuvutia zaidi na zinatoka katika nchi ya Sri Lanka katika mmea ujulikanao kama Cinnamon Zeylanicum. Hujulikana pia kama mdalasini wa India.

Huwa na rangi ya kahawia (light brown), mwembamba na mlaini.

(b) Cassia cinnamon; wakati mdalasini feki ni sumu, pia inajulikana kama ‘Cassia cinnamon’ ni mdalasini huu ambao katika baadhi ya nchi umepigwa marufuku kutumika wala kuingizwa nchini mwao. Hujulikana pia kama mdalasini wa China na wengine huuita Saigon.

Mdalasini huo unatoka katika nchi za China, Vietnam na Indonesia. Wenyewe huwa una joto zaidi na huwa na ladha kali na ya kuwasha ukiutumia. Madhara yake ni pamoja na kudhuru ini na figo ukitumika kwa kipindi kirefu.

Cassia cinnamon huuzwa bei rahisi sana na mwingi unaopatikana huko masokoni. Huwa na rangi inayokaribia na uweusi.

Kwa kawaida ni vigumu kutofautisha aina hizi mbili za mdalasini ukishakuwa tayari katika mfumo wa unga tofauti na ukiwa bado katika fimbo au magome. Nunua kutoka kwa mtu unayemuamini zaidi.

5. Kula vyenye vitamini B; ili kuzuia ganzi mwilini hasa kwenye mikono na miguu ni muhimu kwamba unakula vyakula zaidi vyenye vitamini B kwa wingi hasa vitamini B6 na B12.

Vitamini hizi ni muhimu kwa ajili ya afya nzuri kuzipa neva uwezo wa kufanya kazi vizuri na upungufu wake unaweza kusababisha ganzi katika sehemu mbalimbali za mwili kama kwenye mikono, vidole na miguu.

Vyakula hivyo ni pamoja na mayai (mayai ya kuku wa kienyeji), parachichi, nyama, maharage, samaki, maziwa, mtindi, mbegu mbegu nk

Unaweza pia kutumia vitamini B-complex mara 2 kwa siku kila siku. Kwa dozi sahihi zaidi muulize daktari wako wa karibu.

6. Ongeza matumizi ya magnesiamu

Usawa mdogo wa magnesiamu katika mwili ni moja ya sababu ya kutokea kwa ganzi katika sehemu mbalimbali za mwili. Magnesiamu ni madini muhimu katika kuwezesha ufanyaji kazi ulio mzuri wa neva za mwili na mzunguko mzuri wa damu mwilini.

Kula vyakula vyenye magnesiamu zaidi kama vile mboga za majani zenye rangi ya kijani, mbegu mbegu, siagi ya karanga, soya, parachichi, ndizi, chokoleti nyeusi, na mtindi wenye mafuta kidogo.

Unaweza pia kutumia viinilishe vya magnesiamu gramu 350 kila siku ila ongea kwanza na daktari wako wa karibu.

Vingine muhimu vya kuzingatia

1. Kuwa ‘bize’ na mazoezi kila siku.2. Usikae muda mrefu kwenye kiti.3. Epuka chai ya rangi, kahawa, soda nyeusi na vinywaji vyote vyenye kaffeini.4. Kula zaidi matunda na mboga za majani5. Kunywa maji mengi kila siku kidogo kidogo kutwa nzima6. Epuka sigara na bidhaa nyingine za tumbaku.7. Vaa viatu ambavyo ni saizi yako pia epuka viatu vyenye visigino virefu zaidi8. Hakikisha una uzito sahihi na siyo uliozidi

Wasiliana na Fadhili Paulo, Tabibu wa Tiba Asilia kwa ushauri zaidi; WhatsApp +255769142586.


Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad