Afisa wa Zanu-PF amesema kuwa hoja ya kumnyang’anya urais itawasilishwa bungeni leo Jumanne na mchakato wa kumg’oa madarakani unaweza kuchukua siku mbili tu.
Mashtaka yaliyomo kwenye hoja hiyo ni pamoja na kiongozi huyo mwenye umri wa miaka 93 “kumpa madaraka makubwa ya kikatiba mkewe Grace, na kushindwa kuheshimu katiba”.
Viongozi wa kijeshi , ambao wiki iliyopita waliingilia kati kuchukua mamlaka ya nchi walisema atakutana na makamu wake wa rais wa zamani aliye uhamishoni karibuni.
Jeshi limesema kuwa lina mpango na Mugabe kuhusu hali ya baadae.
Jumapili, licha ya shinikizo kubwa Mugabe aliwashangaza wengi kwa kukataa kujiuzulu, na badala yake katika hotuba yake kupitia televisheni alisema kuwa ataongoza mkutano mkuu wa chama Zanu-PF.