Mwanadada ambaye jina lake kwa sasa kwenye ulimwengu wa mitindo lipo juu, Hamisa Mobeto, hivi karibuni amechukua nafasi ya kuzungumziwa zaidi baada ya kudaiwa kukumbwa na gonjwa hatari lililosababisha akili zake kuruka, Ijumaa linakupa stori zaidi.
Baada ya taarifa hiyo kusambaa kwenye mitandao ya kijamii na mitaani kuanza kuwa gumzo, Ijumaa liliamua kuzifungia kazi na kumtafuta mwanamitindo huyo ili aweze kufungukia madai hayo pamoja na kufahamu kama ni kweli alikuwa mgonjwa au la!
Paparazi wetu walimsaka Mobeto kwa njia ya simu ya mkononi kwanza hakufanikiwa kumpata ndipo alipoamua kumtwangia simu mama yake ambaye alikuwa hewani. Baada ya simu ya mama Mobeto kuita kwa sekunde kadhaa aliweza kuipokea na kusikiliza kile ambacho paparazi wetu alikuwa akimuelezea kuhusiana na madai mbalimbali yakiwemo ya madai ya afya ya akili alimjibu mwandishi wetu; “Wewe si ndiye ulileta uchawi hapa nyumbani,” kisha akakata simu.
Hata hivyo, jitihada za kumsaka Mobeto hazikuweza kukoma ambapo lilimpigia simu yake ya mkononi ambapo wakati huu iliweza kuita.
Mobeto alipopokea simu yake aliweza kupongezwa kutokana na tuzo aliyojishindia hivi karibuni nchini Afrika Kusini, na baada ya hapo alisomewa madai ya kwenye mitandao ya kijamii kuhusu kuugua uchizi na kupokonywa mtoto wake wa kike aitwaye Fantancy na mzazi mwenza. “Aisee mitandaoni kweli kuna mambo, mimi kuumwa uchizi?
Ishu ipo hivi, kiukweli nilikuwa ninaumwa (sio uchizi), nikawa ndani kwa siku kama mbili hivi, lakini kawaida tu kama ambavyo anaweza kuumwa mtu mwingine lakini hilo la uchizi mimi silielewi,” alisema Mobeto. Kuhusu mtoto wake, alisema hajanyang’anywa isipokuwa amekwenda tu kwa baba yake.
Stori: Mayasa Mariwata na Boniface Ngumije
Chanzo: Global Publishers