Mganga Mkuu Hospitali ya Rulenge Sr Goleth Fredrick amesema idadi hiyo imeongezeka baada ya wengine kutolewa katika kituo cha afya Bukiriro na kwamba wanafunzi watatu wamefariki na kufikisha idadi ya vifo vya wanafunzi sita.
Kamanda wa Polisi mkoani Kagera Agustino Olomi amesema chanzo cha wanafunzi hao kujeruhiwa kwa bomu ni baada ya mmoja wao kuliokota akidhani ni chuma chakavu.
“Mmoja wapo aliliokota akidhani kwamba ni chuma chakavu hivyo akaamua kuja nalo shuleni baadaye alipeleke kwa mnunuzi ili aweze kununua madaftari’’amesema
Hata hivyo kamanda wa Kikosi cha Kulinda mipaka cha jeshi la wananchi wa Tanzania JWTZ wilaya ya Ngara meja Mutaguzwa amesema bomu hilo lilikuwa na vipande 36 na lingelipukia ndani ya darasa lingeleta athari zaidi .
Mganga Mkuu wa Hospitali ya Misheni Rulenge, Goreti Francis amethibitisha kupokewa miili ya wanafunzi hao waliopoteza maisha.
“Majeruhi wana majeraha sehemu mbalimbali za mwili, tunafanya kila jitihada kuokoa maisha yao,” amesema Dk Francis.
Akizungumza kwa simu akiwa eneo la tukio, zaidi ya kilomita 50 kutoka Ngara mjini, diwani wa Kibogora, Adronis Bulindoli amesema wanafunzi waliofariki wana umri kati ya miaka minane na tisa.