Ikitokea Nimetimukliwa Simba Wala Sitoshtuka.- Omog

Ikitokea  Nimetimukliwa Simba  Wala Sitoshangaa- Omog
LICHA ya kuwepo kwa tetesi nyingi zikimhusisha Kocha Mkuu wa Simba, Mcameroon, Joseph Omog, kutaka kutimuliwa kikosini hapo, mwenyewe ameibuka na kusema kuwa, ikitokea hivyo wala hatashtuka.

Hivi karibuni, kumekuwa na taarifa nyingi za chinichini zikimhusisha kocha huyo kutaka kutimuliwa kutokana na kile kilichoelezwa kushindwa kupanga kikosi cha ushindi kwenye baadhi ya mechi za Ligi Kuu Bara licha ya kuwa na wachezaji wengi mahiri.

Katika usajili wa dirisha kubwa uliofungwa Agosti 6, mwaka huu, Simba ilisajili wachezaji 14, hali ambayo inaifanya timu hiyo kuwa na nyota wengi wazuri akiwemo Haruna Niyonzima na Emmanuel Okwi. Licha ya kujaza nyota wengi kama hao, lakini Simba katika baadhi ya mechi imekuwa haipati matokeo ya kufurahisha jambo ambalo limetafsiriwa moja kwa moja kuwa Omog ameshindwa kukiongoza kikosi hicho.

Wakati tetesi hizo zikizidi kuenea, Simba ilimleta nchini kocha Masoud Djuma raia wa Burundi ili awe msaidizi wa Omog baada ya kuondoka kwa Mganda, Jackson Mayanja, lakini imeelezwa kuwa, pindi Omog akiondoka, Mrundi huyo atachukua mikoba hiyo kwani alipokuwa akiinoa Rayon Sports kabla ya kutua Simba, alikuwa kocha mkuu.

Akizungumzia mustakabali wake ndani ya Simba, Omog amesema: “Kwa sasa naona naifanya kazi yangu kwa ufasaha kwani ukiangalia msimamo tupo vizuri tu na wala si sehemu mbaya. “Makocha wengi wamekuwa wakitimuliwa kwenye timu zao, hivyo wala sihofi i ikitokea jambo hilo kwa sababu naamini hakuna nilichoshindwa kukifanya, kama ushindi tunapata.”
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad