Imebainika...Polisi, Mahakama vinara wa Rushwa Tanzania

Utafiti wa shirika lisilo la kiserikali la Twaweza umebaini kuwa Idara za Polisi na Mahakama bado zinaongoza kwa rushwa, licha ya kuwa ni taasisi zinazohudumia idadi kubwa ya watu.

Hayo yamebainishwa kwenye uzinduzi wa ripoti ya utafiti huo iliyopewa jina "Hawashikiki" uliofanyika leo jijini Dar es Salaam na kuhudhuriwa na wadau kutoka sekta za umma na kibinafsi.
Kwa mujibu wa matokeo ya utafiti huo, wananchi wanaripoti kuwa licha ya viwango vya rushwa kupungua nchini kwa mwaka huu, bado idara za polisi na mahakama zimeendelea kuwa na kiwango kikubwa cha rushwa ambapo kati ya 36% na 39% ya wananchi waliohojiwa, wameiambia Twaweza kuwa waliombwa rushwa mara ya mwisho walipofika katika taasisi hizo.

Hata hivyo Mkurugenzi wa Utetezi wa Twaweza Bi. , Anastazia Lugaba, amesema kuwa wananchi walitoa rushwa ili kupata huduma ya uhakika katika sekta hizo lakini kwa sauti za wananchi zinazoonesha matumaini katika mapambano dhidi ya rushwa.

Ndani ya utafiti huo pia wananchi wamezungumzia sakata maarufu la kampuni ya madini ya Acacia wakiliweka katika kundi la rushwa kutumika kwa kiasi kikubwa, huku Mamlaka ya Mapato ya Tanzania pamoja na Mamlaka ya Bandari nazo zinaonekana kushughulikiwa ipasavyo na Taasisi ya Kuuzuia na Kupambana na Rushwa Takukuru huku wakitaja vyama vya upinzani vingelifanya vizuri zaidi katika kupambana na rushwa endapo vingepata nafasi ya kuwa madarakani .
Tags

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Tatizo huyo mdudu rushwa alianza kutafuna tangia enzi za Biblia, manake hata YUDA Iskariote alitafunwa na matokeo yake akamuuza MASIHI, Jitihada kubwa zinahitajika kupambana nae, Inshaallah anaweza akatokomezwa. Kwa yakini kinachokesekana ni utu kwa hao wapokea rushwa na si suala la udogo wa mishahara, wapo watu wenye mishahara midogo sana lakini ni waadilifu na hawapokei rushwa ilhali hao wenye mishahara mikubwa ndio wapokeaji wakubwa wa rushwa.

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad