Siku ya jana ilikuwa ya kipekee sana baada ya Makamu wa Rais, Samia Hassan kuamua kumtembelea hospitalini Nairobi kwenda kumpa pole, mbunge huyo wa Singida Mashariki, baada ya kupigwa risasi zaidi ya 30, mchana kweupe, zaidi ya miezi 2 na nusu iliyopita.
Nimesema ni tukio la kihistoria kwa kuwa huyo ni kiongozi wa kwanza wa juu, kutoka Chama Cha Mapinduzi kwenda kumtembelea Tundu Lissu.
Tanzania ya sasa tumejenga utaratibu mpya, ambapo janga kama limekukuta mtu wa upinzani, inakuwa kama hairuhusiwi kwa viongozi wa upande
wa CCM kwenda kumuona, na ukienda kumwona utahesabika ndani ya Chama chako kama msaliti!
Tulishuhudia wakati mbunge wa Arusha mjini, Godbless Lema alipokuwa rumande kwa miezi 4 mfululizo ambapo hakuna kiongozi yeyote kutoka CCM aliyekwenda kumwangalia gerezani Kisongo.
Najua kibinadamu wapo wanaccm wengi wanaumia sana kwa yaliyomkuta Tundu Lissu, lakini kwa msimamo wa Chama chao, wanahofia kwenda kumwona Tundu Lissu, kwa kile kinachoonekana kuwa wataitwa wasaliti!
Kwa kweli siyo utamaduni wa mtanzania, kubaguana kiasi hiki, kwa janga linalokukuta mtu wa upinzani iwe ni "marufuku" kwa kiongozi kutoka Chama Cha Mapindizi kwenda kumfariji.
Ndiyo maana nimesema, je kutokana na Makamu wa Rais, Samia Suluhu kwenda kumwona Tundu Lissu, atakuwa amefungua njia kwa viongozi wenzake wa CCM kwenda kumwona Tundu Lissu hospitalini Nairobi?
Wange anzaje kwenda kumuona wakati hao akina mbowe na kundi lake wanasema serikali ya CCM ndo ilompiga risasi, hivi kama ni wewe ungeweza kwenda kweli au unaropoka tu? Eti walikatazwa kwenda kumuona Lema rumande.....MSIBA-WA-KUJITAKIA-HAUNA-KILIO
ReplyDeleteKabisa.... Swadakta
ReplyDeleteMsumari wa kijitakia hauna ....
Hakwenda kwa ajili yakumsalimia na kumpa pole Lisu, bali alikwenda kwenye sherehe za kuapishwa Kenyata, na kwa kuwa Lisu yupo nairobi akaona bora apitie ili asije akalaumiwa kwamba amefika nairobi lakini hakwenda kumuona Lisu.
ReplyDeleteNdiyo kibinaadamu.
ReplyDeleteAlicho fanya Mama Samia ni Uungwana. Na siyo kuwa ilikuwa Lazima.
Tuna maelfu Muhimbili wa Watanzania na Bugando na KCMC na General Dodoma hata Ntyuka wamelazwa
kwa matatizo tofauti na kila mwenye kupata wasaa wa kuwapitia ndiyo hali ya Uungwana na siyo kuwa ni lazima au ni wajibu.
Mama samia kapita haina maana ilikuwa ni Lazima.....Hapo hakuna Siasa
Wala msiliingize hili katika siasa kama wapendavyo wana Siasa.
Mgonjwa katembelewa kama anavyo tembelewa mgonjwa yeyote.
Dua zenu ndiyo cha muhimu.
Ndiyo kibinaadamu.
ReplyDeleteAlicho fanya Mama Samia ni Uungwana. Na siyo kuwa ilikuwa Lazima.
Tuna maelfu Muhimbili wa Watanzania na Bugando na KCMC na General Dodoma hata MIREMBE wamelazwa
kwa matatizo tofauti na kila mwenye kupata wasaa wa kuwapitia ndiyo hali ya Uungwana na siyo kuwa ni lazima au ni wajibu.
Mama samia kapita haina maana ilikuwa ni Lazima.....Hapo hakuna Siasa
Wala msiliingize hili katika siasa kama wapendavyo wana Siasa.
Mgonjwa katembelewa kama anavyo tembelewa mgonjwa yeyote.
Dua zenu ndiyo cha muhimu.