Jeshi la polisi Lamkamata Mfanyabiashara Anayeuza Risasi Mtaani

Jeshi la polisi Lamkamata Mfanyabiashara Anayeuza Risasi Mtaani
Jeshi la Polisi Kanda Maalum Dar es Salaam,limesema kuwa tarehe 6, Novemba mwaka huu maeneo ya Serengeti Kigamboni lilipokea taarifa ya kuwepo kwa mtu mmoja anayefahamika kwa jina la Willy Peter kuwa anafanya biashara ya kuuza risasi mtaani. Polisi walifanya ufuatiliaji na hatimaye kufanikiwa kumkamata mtuhumiwa huyo akiwa na risasi 69 za kivita aina ya FN G3.
Katika mahojiano mtuhumiwa huyo alikiri kuwa risasi hizo alipewa na mtu aliyemtaja kwa jina la Matabu William kwaajili ya kwenda kuziuza na kwamba alimpatia risasi hizo huko nyumbani kwake Kiwalani jijini Dar es salaam.

Hata hivyo polisi walifika nyumbani kwa Matabu William Matoke (52) kiwalani ambapo alikiri kufanya biashara hiyo ya risasi na alipopekuliwa katika nyumba yake hiyo alikutwa na risasi moja aliyokuwa ameifukia pembezoni mwa nyumba yake na kufanya jumla ya risasi zilizokamatwa kuwa 70.

Aidha Kamanda Mambosasa amesema kuwa watuhumiwa wote wawili wanaendelea kuhojiwa zaidi na upelelezi utakapokamilika hatua za kisheria zitachukuliwa dhidi yao.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad