Kampuni ya udalali ya YONO asubuhi ya leo November 9, 2017 imeifunga Hotel ya Blue Pearl iliyopo kwenye jengo la Ubungo Plaza Ubungo Dar es salaam kutokana na Mmiliki wake kudaiwa kodi ya pango.
Boss wa YONO amenukuliwa akisema Mmiliki wa Hoteli hiyo anadaiwa kodi ya pango ya bilioni 5 na Milioni 700 za Kitanzania ambapo wakati wanakwenda kumfungia asubuhi hii Wageni walikuwepo vyumbani na ikawalazimu waondolewe kuhamishiwa kwenye Hoteli nyingine.
Kampuni ya Umma ya Ubungo Plaza Limited inayomilikiwa kwa ubia na Kampuni kubwa tatu NSSF, PSPF na NIC ndio inayomiliki jengo hilo ambapo Mkurugenzi Mtendaji wa Ubungo Plaza Haroon Mgube amesema Blue Pearl alikua akilipa kodi ya pango vizuri tu kuanzia mwaka 2006 mpaka 2014.
Blue Pearl Hotel ilikua na mkataba wa miaka 15 kukaa kwenye jengo hilo na mkataba huo ungeisha 2021 lakini kutokana na kushindwa kulipa kodi ya pango kwa miaka iliyofatia, ameondolewa leo kwa nguvu huku mali zake zikishikiliwa.
Jina la Hoteli ya Blue Pearl Lafutwa, Wageni Waondolewa
0
November 04, 2017
Tags