Kagasheki Amjia Juu Kigwangala " Naomba Athibitishe Ukaribu Wangu na OBC, Vitalu Nilivogawa Nikiwa Waziri na Rushwa Niliyopokea"

Kagasheki Amjia Juu Kigwangala " Naomba Athibitishe Ukaribu Wangu na OBC, Vitalu Nilivogawa Nikiwa Waziri na Rushwa Niliyopokea"
Aliyekuwa Waziri wa Maliasili na Utalii Balozi Khamisi Kagasheki amemvaa Waziri wa sasa wa sasa wa wizara hiyo Mh. Hamisi Kigwangalla kwa kumtaja kuwa ana mahusiano ya karibu na Mkurugenzi wa OBC ambaye ana kashfa kubwa ya rushwa.
Kupitia mtandao wake wa Twitter Balozi Kagasheki alimtaka Mh. Kigwangalla amthibitishie kuhusu ukaribu wake na Mkurugenzi huyo na kuhusu rushwa aliyowahi kupokea ikiwa ni pamoja na kuuza vitalu.
Balozi ameandika "Waziri wa Maliasili na Utalii Hamisi Kigwangalla alinukuliwa kutaja "muwekezaji OBC" alivo na kashfa za Rushwa. Alinitaja mimi kuwa karibu na OBC. Napenda athibitishe ukaribu huo, vitalu nilivogawa nikiwa Waziri na rushwa niliyopokea," Balozi Kagasheki
Hata hivyo baada ya ujumbe huo ambao ulienda moja kwa moja kwa Waziri Kigwangalla naye alijibu ujumbe huo ambao ulielekezwa kwake na kumuomba Mstaafu huyo wayazungumze nje ya mtandao
"Mhe. Balozi Kagasheki , wewe ni kaka yangu na unajua nakuheshimu sana. Tuongee kindugu nje ya hapa! Kuweka sawa ni kwamba 'sikukutaja!" Kigwangalla.
Hivi karibuni Waziri Kigwangalla aliweka wazi kwamba amewaondoa Askari wote wa kituo cha Geti la Kleins kwa kuwa wamekuwa wakitumika na mwekezaji huyo ambaye ana uhusiano wa Karibu na Prof. Songorwa (aliyemsimamisha kazi siku chache zilizopita) na alikuwa na uhusiano ya karibu na Prof. Maghembe, Lazaro Nyalandu, balozi Kagasheki na Mawaziri wa Maliasili na Utalii wa zamani.
Balozi Kagasheki aliwahi kuwa Waziri wa Maliasili na Utalii katika uongozi wa serikali ya awamu ya nne ambapo aliongoza wizara hiyo Mwaka  (2012-2013)
Tags

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Ni wanachama wa ccm mmoja zidi ya mwenzie.bado wanachama viongozi wa ccm wanapikuana tu. Kisa cheo. Na hii inaumiza Taifa. Hwa viongozi hawana sifa, wanateuliwa bila uwezo wa kazi, ni kama favoritism wanapeana wao kwa wao huku wakicopete wao kwa wso. Hawapo kwa manufaa ya watanzania. Ni kijani wamepewa pass na raisi.wanajua wapo above the law kulinganisha na chama kingine chochotewanalichezea Taifa tu.

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad