Katambi Amjibu Mbowe, Amwambia Hanunuliki

Aliyekuwa Mwenyekiti wa Baraza la Vijana la Chadema (Bavicha), Patrobas Katambi amesema tuhuma zinazoelekezwa kwake kwamba amenunuliwa na Chama Cha Mapinduzi (CCM) hazina ukweli.

Katambi ambaye jana alitangaza kujiunga na CCM ametoa kauli hiyo kipindi ambacho kumekuwa na tuhuma zinazoelekezwa kwake  ikiwamo ya Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe kwamba ameshawishiwa na akakubali.

Akizungumza na Mwananchi leo Novemba 22, Katambi amesema hakuna mtu yoyote anayeweza kumnunua huku akisema Chadema kimepoteza dira hivyo wenye uelewa wataondoka.

“Nimesikia mengi, nitafanya mkutano na waandishi wa habari, nilidhani wangejitathimini katika ukweli ili kusaidia vijana, chama na taifa lakini kama wanaamua kushambulia mtu kwa uongo bila ushahidi, nitasema ukweli waziwazi,” amesema Katambi

Kuhusu tuhuma za rushwa, Katambi amesema ‘’Katambi hanunuliki wala hana bei naishi katika Principle…kwa wenye akili wangejua dira imepotea watafute upya masafa.”

Awali leo asubuhi, Mbowe ambaye ni Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni akizungumza  na Mwananchi kuhusu kuondoka kwa Katambi amesema;

"Badala ya nguvu na fedha kuzielekeza kujenga viwanda wao nguvu wamezielekeza kushawishi viongozi wetu, wamewashwishi wengi na Katambi ni miongoni ingawa wengine wamekataa."

Mwananchi:
Tags

Post a Comment

3 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Wananchi ndio wataamua kama kweli chadema imepoteza mwelekeo na Sio wewe mtu mmoja uliyehama .Ila Mimi kwa maoni yangu naona chadema kama kipindi hiki ndio inaeleweka.jibu tusubiri uchaguzi wa udiwani

    ReplyDelete
  2. Kama ana utu hangepayuka. Ni vijana wenye njaa wakifikiri mabadiliko ni rahisi na wanarudi kulekule kulikowanyonya, waibia, kusiko na maadili. Inasikitisha. Walionyesha ushujaa kumbe sio. Wamemuacha Mbowe kitandani kutafuta kula. Ndo huu uzaleno wanaouita. Vyama vingi bila elimu ya kujua nini wakipiganiacho na muda gani ili nchi ibadilike. Hawana subira. Hekima hakuna. Ukiangalia nchi nyingine mawazo ya kichama hayabadiliki namna hii kwa kuigana .ameanza moja mia wanafuata. Inaoneksna bado watu hawajui uzalendo ni nini. Bado wanahangaika na maidha binafsi. Mtu unapigania haki mpaka ushinde.sijawahi kuona nchi hata moja duniani vijana wanayumba namna hii.nchi bado kaijajitambua na tutaingia tu tena kubaya kama vijana wetu ndo hivi wa kuyumbishwa kwa kitu kidogo.
    Bongo, ukisikia Bongo ni Bongo kwelikweli.tuione hii ccm iliyokataa kurudisha katiba eti inawafanyia kazi watanzania. Wasiojiweza hata kjilipia hospitali kuwategemea wachina .kama haya ndio maendeleo watanzania wanayataka basi ni hayo tuone yatadumu mpaka lini.bado tutazidi kuwa tsifa tegemezi ingawa tajiri fikra finyu, uhodari hatuna wa kupigania ukweli, eoga mwingi umetujaa.

    ReplyDelete
  3. Aibu sana kitambi.mtu unapopewa cheo kikubwa inabidi uwe na utu na hadhi.kuna vitu inabidi ukae navyo moyoni. Kwa hivi ukihama ccm domo utalifungua tena badala ya kuangalia dhamira yako kama i safi. Ni rahisi kumnyoshea mtu mwingine vidole tazama vingapi vinakusuta.huna hekima.huwezi kumdharalisha Mbowe mtu anayejiamini. Wewe hujiamini ulibebwa na wengi ukang'alishwa. Umesahau.

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad