Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imeahirisha kesi ya kumiliki mali na kuishi kifahari kinyume na mshahara wake inayomkabili Ofisa Msaidizi wa Forodha wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Jennifer Mushi hadi December 12, 2017 kwa sababu upande wa mashtaka haujamaliza kuandaa maelezo ya awali (PH).
Wakili wa Serikali, Vitalis Peter amemueleza Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shaidi kuwa kesi hiyo imeitishwa kwa ajili ya kusomewa maelezo ya awali (PH) lakini bado hawajamaliza kuandaa.
“Tunaomba tupangiwe tarehe nyingine ili tuje kumsomea mshtakiwa maelezo yake,” alieleza Peter.
Baada ya kueleza hayo, Hakimu Shahidi ameahirisha kesi hiyo hadi December 12,2017.
Mshtakiwa ana makosa mawili, inadaiwa kati ya March 21, 2016 na June 30, 2016 katika maeneo tofauti ya Jiji la Dar es Salaam,akiwa mwajiriwa wa TRA, kama Ofisa msaidizi wa forodha alikutwa akimiliki mali zisizolingana na kipato chake, kinyume na sheria.
Inadaiwa alikutwa akimiliki magari 19 ambayo ni Toyota ra4,Toyota dyna truck, Toyota viz, Suzuki carry,Toyota ipsum,toyosha wish,Toyota mark ll,Toyota regiusage,Toyota estima,Toyota Alex,Toyota Noah,Toyota crown,Toyota hiace,Toyota estima,Toyota lasso,Suzuki carry, ambayo yana thamani ya Tsh.197.6.
Kosa la pili, anadaiwa kuwa kati ya March 21, 2012 na March 30, 2016 jijini Dar es salaam akiwa mwajiri wa TRA aliishi maisha ya kipato cha juu tofauti na kipato chake yenye thamani ya Tsh. 333,255,556.24 tofauti na kipato chake.
Mshtakiwa yupo nje kwa masharti ya dhamana ya kuwa na mdhamini mmoja aliyesaini bondi ya Tsh. milioni 20
Kesi Inayomkabili Mfanyakazi wa TRA ya Kumiliki Mali na Kuishi Kifahari Kinyume na Mshahara Wake Imeahirishwa
0
November 07, 2017
Tags