Kigogo wa ESCROW Ameachiwa Huru na Mahakama

Kigogo wa ESCROW Ameachiwa Huru na Mahakama
 Mahakama  Kisutu imemuachia huru aliyekuwa Mkurugenzi wa Huduma za Sheria wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Rugonzibwa Mujunangoma ambae alikua anakabiliwa na kosa la kupokea rushwa ya Sh. milioni 323 kutoka kwa Mfanyabiashara James Rugemalira.

Taarifa inaeleza zaidi kwamba fedha hizo zilikua ni sehemu ya fedha za Akaunti ya Tegeta ESCROW ambapo kigogo huyo ameachiwa na hakimu Mkazi Mwandamizi Victoria Nongwa baada ya Mwendesha Mashtaka Mwandamizi wa TAKUKURU, Leonard Swai kuomba kesi hiyo iondolewe Mahakamani chini ya kifungu cha 98 (a) cha  sheria ya Makosa ya Jinai (CPA).

Baada ya kueleza hayo, Hakimu Nongwa alisema Mshtakiwa huyo amefutiwa kesi na kwa sasa yupo huru ambapo kama utakumbuka, Rugonzibwa alifikishwa Mahakamani kwa Mara ya kwanza January 14, 2015 na Taasisi ya Kuzuia na Kupamba na Rushwa (TAKUKURU).

Inadaiwa alipokea rushwa hiyo ya milioni 323 kutoka kwa Rugemalira ambae alikuwa ni mshauri huru wa kitaalamu, Mkurugenzi wa VIP na mkurugenzi wa zamani wa Kampuni ya Kufua Umeme ya IPTL kama tuzo kwa kushughulikia mambo ya ufilisi wa muda wa kampuni hiyo.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad